-
SEPAH: Tunaiunga mkono harakati yoyote inayopambana na Uzayuni duniani
Apr 14, 2022 05:54Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, tunaiunga mkono harakati yoyote inayopambana na utawala wa Kizayuni duniani na uungaji mkono huo utaendelea.
-
Ershadi: Ugaidi na uvamizi wa kigeni ni vitisho vikubwa kwa usalama wa wanawake
Apr 14, 2022 02:31Zahra Ershadi, balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa: "Kuzikalia kwa mabavu ardhi za mataifa mengine, uvamizi wa kigeni na ugaidi ndio vitisho vikuu kwa usalama wa wanawake katika Asia Magharibi."
-
Ubalozi wa Iran mjini London wakanusha ripoti ya Guardian kuhusu silaha za Iran kutumwa Russia
Apr 13, 2022 21:55Ubalozi wa Iran mjini London umekanusha ripoti ya gazeti la Guardian la Uingereza inayodai kwamba Russia imetumia silaha zinazodaiwa kutoroshwa na Iran kutoka Iraq.
-
Iran: Tumejiandaa kikamilifu kukabiliana vilivyo na vitisho vya maadui
Apr 13, 2022 07:03Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, majeshi ya Jamuri ya Kiislamu ya Iran yako imara na yamejiandaa kikamilifu kukabiliana vilivyo na vitisho vya maadui.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu ulazima wa kukomeshwa vita vya Yemen
Apr 13, 2022 06:42Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Jumanne jioni akizungumza katika kikao cha viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa mfumo wa Kiislamu, ameashiria na kufafanua masuala mbalimbali katika uga wa ndani na nje ya nchi.
-
Kiongozi Muadhamu: Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umeyavutia mataifa mengi duniani
Apr 12, 2022 23:38Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema changamoto zote zinazolikabili taifa hili zinaweza kupatiwa ufumbuzi na kusisitiza kuwa, Mfumo wa Uongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umepata mafanikio mengi katika sekta tofauti na kuwa kivutio kikubwa kwa mataifa mengi duniani.
-
Iran yataka mzingiro dhidi ya Yemen uondolewe kikamilifu
Apr 12, 2022 23:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza ulamiza wa kuondolewa kikamilifu mzingiro dhidi ya Yemen na kufikiwa mapatano ya kudumu ya usitishwaji vita ili hatimaye mazungumzo ya amani ya Wayemen yaanze.
-
Burkina Faso yaomba uzoefu wa Iran katika mapambano dhidi ya ugaidi
Apr 12, 2022 03:21Waziri mpya wa Mambo ya nje wa Burkina Faso ameiomba Iran, kama nchi ambayo imeathiriwa na ugaidi kwa miaka mingi, kuipatia Ouagadougou uzoefu wake katika uwanja huo.
-
Khatibzadeh: Marekani bado haijaonyesha nia ya kufikia makubaliano
Apr 11, 2022 03:48Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema kuwa, Marekani bado haijaonyesha nia ya kutosha ya kufikia makubaliano katika mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea huko Vienna nchini Austria na kuongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiathiriwi na kampeni za vyombo vya habari na matamshi yanayokinzana.
-
Iran yaikosoa Marekani kwa kuibua masharti mapya ya kuondoa vikwazo
Apr 10, 2022 22:06Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Marekani imeibua masharti mapya inayotaka Tehran itekeleze ili iondolewe vikwazo sanjari na kuhuishwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ya mwaka 2015.