-
Hafla za maombolezo Iran kwa mnasaba wa Tasu'a ya Imam Hussein AS
Aug 18, 2021 00:02Katika usiku wa kuamkia Tasu'a ya Imam Hussein AS, taifa lote la Iran limeghiriki katika maombolezo kwa mnasaba wa siku hii.
-
Rais Ebrahim Raisi: Nchi za Asia Magharibi zinaweza kubuni ramani ya njia ya amani bila ya kutegemea madola ya kigeni
Aug 17, 2021 11:26Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa nchi za eneo la Magharibi mwa Asia zinaweza kubuni ramani ya njia na kuimarisha amani, utulivu na usalama endelevu kwa kushirikiana, na kuongeza kuwa uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya eneo hilo hauwezi kudhamini amani, ustawi na maendeleo.
-
Salami: Tutatumia uwezo wetu kustawisha Iran
Aug 17, 2021 03:01Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Brigedia Jenerali Hussein Salami amesisitiza kuwa, taifa la Iran linamtegemea Mwenyezi Mungu na nguvu zake za ndani na kuongeza kuwa, 'tutatumia uwezo wetu wote kwa ajili ya ustawi wa watu wa Iran."
-
Khatibzadeh: Iran itatumia uwezo wake kuleta maelewano Afghanistan
Aug 16, 2021 23:32Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatumia uwezo wake wote kwa ajili ya kuhimiza mazungumzo na maelewano nchini Afghanistan.
-
Rais Raisi: Iran inafanya jithada ili kurejesha utulivu Afghanistan
Aug 16, 2021 07:28Rais Ebrahim Raisi amesema, Iran itafanya jitihada kurejesha utulivu na uthabiti nchini Afghanistan ambalo ndilo hitajio la kwanza la nchi hiyo kwa sasa.
-
Iran yatangaza uungaji mkono wake kwa taifa la Afghanistan
Aug 16, 2021 03:17Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu kama ilivyofanya katika kipindi cha miaka 40 iliyopita, vivyo hivyo itaendelea kuwaunga mkono wananchi wa Afghanistan na matakwa yao.
-
Zarif: Iran itaendeleza jitihada za kusaidia kupatikana amani Afghanistan
Aug 15, 2021 23:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itaendeleza jitihada za kuhakikisha kuwa amani na maridhiano yanapatikana nchini Afghanistan.
-
Raisi: Ununuzi wa dozi milioni 30 za corona tayari umeidhinishwa
Aug 14, 2021 05:35Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Corona kwamba tayari ameidhinisha kununua dozi milioni 30 za chanjo ya corona.
-
Bunge la Iran laanza kuchunguza sifa za mawaziri waliopendekezwa na Rais Raisi
Aug 14, 2021 03:38Msemaji wa kamati ya uongozi ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, bunge hilo linaanza mchakato wa kuchunguza sifa za mawaziri wa serikali mpya waliopendekezwa na Rais Ebrahim Raisi.
-
Araqchi: Uingereza haitaweza katu kuirubuni Iran kimabavu
Aug 14, 2021 03:15Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, Uingereza inafanya kila njia ili kuirubuni Iran kimabavu mkabala wa kulipa fedha za madeni inayodaiwa na Iran, ambazo inazishikilia kinyume cha sheria kwa zaidi ya miaka 40 sasa.