-
Velayati: Iran itaendelea kuunga mkono taifa la Palestina
May 17, 2021 03:52Mshauri mkuu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amesema kwamba Waislamu wote ulimwenguni wana jukumu la kutetea na kuwaunga mkono Wapalestina wanaokandamizwa kila uchao na utawala wa kigaidi wa Israel. Akisisitiza suala hilo, Ali Akbar Velayati amesema kwamba Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kutetea na kuwaunga mkono Wapalestina bila uoga wowote.
-
Hatibzadeh: Hakuna "mapatano ya awali" katika mazungumzo ya nyuklia ya Vienna
May 17, 2021 03:32Msemaji wa Wizara Ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amesema kuwa, hakuna suala linalotajwa kama "mapatano ya awali" katika mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea huko Vienna, Austria, na kwamba asilimia kubwa ya masuala yaliyobaki yamekamilishwa kna yanasubiri maamuzi ya kisiasa.
-
Rouhani: Kadhia ya Palestina ni muhimu zaidi kwa umma wa Kiislamu
May 16, 2021 22:27Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na mwenzake wa Uturuki na kusisitiza kuwa kadhia ya Palestina ni kadhia muhimu zaidi kwa umma wa Kiislamu hivi sasa.
-
Zarif: Kunahitajika kampeni iliyoratibiwa ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni
May 16, 2021 22:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuna haja ya kuwepo kampeni iliyoratibiwa kisheria na ya kisiasa kwa lengo la kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel kieneo na kimataifa.
-
Dozi 162,000 za chanjo ya COVID-19 zinatolewa Iran kwa siku
May 16, 2021 22:19Waziri wa Afya wa Iran Daktari Saeed Namaki amesema hivi sasa Iran inatoa dozi 162,000 za chanjo ya COVID-19 kwa siku.
-
Zarif ashiriki kikao cha dharura cha OIC kuhusu Palestina, Iran yailaumu UN kwa undumilakuwili
May 16, 2021 07:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameshiriki katika kikao cha dharura kilichofanyika kwa njia ya Intaneti cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC cha kuzungumzia Palestina na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Spika wa Bunge la Iran: Umma wa Kiislamu utalitetea kwa nguvu zote taifa la Palestina
May 16, 2021 03:46Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu nchini Iran (Bunge) amesema kuwa moyo wa Umma wa Kiislamu unaendelea kudunda kwa ajili ya Palestina, na Umma na makundi ya mapambano dhidi ya Uzayuni yataendelea kusimama kidete na kutetea malengo ya ukombozi wa Palestina.
-
Zarif afuta safari yake Austria akipinga kuwekwa bendera za Israeli kwenye majengo ya serikal
May 16, 2021 00:02Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amefuta safari yake rasmi nchini Austria akipinga hatua ya nchi hiyo ya kupeperusha bendera za utawala haramu wa Israel juu ya majengo ya serikali katika mji mkuu wa nchi hiyo Vienna, huku Israel ikiendelea kuwaua kinyama raia wa Palestina.
-
Zoezi la kuwasajili wanaotaka kugombea urais Iran laingia siku ya nne
May 14, 2021 03:19Zoezi la kuwasajili wale wanaotaka kuwania urais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeingia siku ya nne leo.
-
Hossein Amir-Abdollahian: muqawama wa Palestina utavuruga mahesabu kwa namna ya kushtua
May 13, 2021 23:01Msaidizi Maalum wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, katika awamu mpya muqawama wa Palestina utavuruga mahesabu kwa namna ya kushtukiza na kushangaza.