-
Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Tehran; kupandishwa uhusiano kati ya Tehran na Beijing hadi kiwango cha ushirikiano wa kistratejia
Mar 27, 2021 06:59Iran na China, zikiwa nchi mbili muhimu na zenye taathira katika mfumo wa kimataifa, zina maslahi na malengo ya pamoja kwa ajili ya kupanua ushirikiano katika nyanja mbalimbali.
-
Iran kuanza kuzalisha chanjo ya Russia ya Sputnik V
Mar 27, 2021 02:45Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuanza kuzalisha chanjo ya COVID-19 ya Sputnik V ya Russia ambayo sasa inataumika katika nchi nyingi duniani.
-
China na Iran kusaini mkataba wa ushirikiano
Mar 27, 2021 02:42Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na China leo Jumamosi zinatia saini mkataba wa ushirikiano wa miaka 25 huku nchi mbili zikiadhimisha miaka 50 tokea zianzishe uhusiano.
-
Ugaidi wa kiuchumi unazuia nchi kadhaa kupata dawa na vifaa vya tiba
Mar 26, 2021 03:06Msemaji wa Tume ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema ugaidi wa kiuchumi unazuia nchi kadhaa duniani kupata dawa na vifaa vya kitiba.
-
Zarif: Kuna upotoshaji mwingi katika hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuhuisha JCPOA
Mar 26, 2021 00:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu madai yaliyo dhidi ya Iran yanayotolewa na wakuu wa nchi za Magharibi dhidi ya Iran na kusema kuna upotoshaji mwingi kuhusu hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kuhuisha mapatano ya nyuklia ya jcpoa.
-
Qalibaf: Stratijia ya baadhi ya nchi ni kutumia ugaidi kwa ajili ya kupeleka mbele malengo yao
Mar 25, 2021 06:01Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa ugaidi na misimamo ya kuchupa mipaka ni tishio la dunia nzima na kusisitiza kuwa, baadhi ya nchi zinatumia ugaidi kama wenzo wa kutimiza malengo ya siasa zao za nje.
-
Iran: Misimamo inayochukuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA ni haribifu
Mar 24, 2021 08:47Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika mashirika ya kimataifa yenye makao yao mjini Vienna amesema kuhusu kauli aliyotoa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA kwamba, kuendelea kuchukua misimamo ya kisiasa badala ya kiufundi, hakujengi bali kunabomoa.
-
Iran: Nchi zinazokanyaga haki za mataifa mengine hazipaswi kujifanya zinaheshimu haki hizo
Mar 24, 2021 02:34Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu azimio dhidi ya Iran lililotolewa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kuwa, nchi zinazokanyaga haki za mataifa ya dunia hazina ustahiki wa kuzungumzia haki za binadamu.
-
Bri. Jen. Hatami: Uingereza ichukue hatua za kivitendo kulipa deni la Iran
Mar 23, 2021 22:39Waziri wa Ulinzi wa Iran ameashiria jinsi Uingereza ilivyokiri kuwa ina deni la miaka 42 la Iran na kuitaka London ichukue hatua za kivitendo za kuilipa Tehran fedha zake hizo ambazo ni mamia ya mamilioni ya dola.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu kuhusu JCPOA; Iran haina haraka
Mar 23, 2021 05:15Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Marekani inapaswa kufuta vikwazo vyote, kisha Iran ichunguze na kutathmini ukweli wa hatua hiyo, na endapo itathibiti kweli kwamba, vikwazo hivyo vimeondolewa, basi taifa hili litarejea bila tatizo lolote katika utekelezaji wa ahadi zake kwa mujibu wa makubaliano hayo.