Iran kuanza kuzalisha chanjo ya Russia ya Sputnik V
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i68346-iran_kuanza_kuzalisha_chanjo_ya_russia_ya_sputnik_v
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuanza kuzalisha chanjo ya COVID-19 ya Sputnik V ya Russia ambayo sasa inataumika katika nchi nyingi duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 27, 2021 02:45 UTC
  • Iran kuanza kuzalisha chanjo ya Russia ya Sputnik V

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuanza kuzalisha chanjo ya COVID-19 ya Sputnik V ya Russia ambayo sasa inataumika katika nchi nyingi duniani.

Kwa mujibu wa Balozi wa Iran nchini Russia Kazem Jalali,  chanjo ya Sputnik V itaanza kuzalishwa nchini Iran mwezi Aprili.

Jalali amesema hivi sasa kuna mashirika mawili ya Iran ambayo yatahusika na mradi huo na kuongeza kuwa, seli za chanjo hiyo ya Russia zitatumwa Iran wiki ijayo ili uzalishaji wa chanjo ya Sputnik V uanze nchini.

Amesema katika awamu ya kwanza, chanjo milioni tisa zitazalishwa nchini Iran katika kipindi cha mwezi mmoja.

Hadi hivi sasa chanjo ya Sputnik V inauzwa katika nchi 57 na hivyo kuifanya kuwa chanjo ya pili kwa umashuhuri duniani.

Shehena ya chanjo ya Sputnik V ya Russia

Katika uchunguzi wa kikliniki uliofanywa, chanjo ya Sputnik V inatoa kinga ya asilimia 91.6 na pia inaweza kukabiliana na aina mpya za kiruis cha COVID-19.

Tayari Iran imeshapokea shehena kadhaa za chanjo ya Sputnik V ambazo zinatumika nchini.