-
Zarif: Magaidi wa Septemba 11 walitoka katika nchi anayoipenda Pompeo
Jan 13, 2021 04:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa radiamali kuhusu madai yasiyo na msingi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye ameifungamanisha Iran na kundi la kigaidi la Al Qaeda na kusisitiza kuwa: "Magaidi wote wa Septemba 11 walitoka katika nchi anazozipenda Mike Pompeo katika Mashariki ya Kati (Asia Magharibi).
-
Zarif: Kurejea Marekani JCPOA bila vikwazo kuondolewa si kwa maslahi ya Iran
Jan 13, 2021 01:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kurejea Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA bila Iran kuondolewa vikwazo ni kwa maslahi ya Marekani ni wala si kwa maslahi ya Tehran.
-
Waziri wa Ulinzi: Maadui wameshindwa kupigisha magoti Iran
Jan 13, 2021 01:12Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Amiri Hatami amesisitiza kuwa, maadui walidhani wangeipigisha magoti Iran lakini wameshindwa kabisa kutokana na Wairani kusimama kidete dhidi yao na sasa ni Rais Trump wa Markeani na waitifaki wake ndio wanaochukiwa zaidi na watu duniani na watatupwa katika dampo la taka za historia.
-
Rabiei: Utekelezaji wa JCPOA hauhitaji mazungumzo mengine
Jan 12, 2021 09:18Msemaji wa serikali ya Iran amezungumzia udharura wa Marekani kusitisha ukiukaji wa majukumu yake ya kimataifa na kueleza kuwa hakuna haja ya kufanya mazungumzo mengine kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ndani ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Iran yasema UN, WHO zinapendelea tekolojia ya Markeani katika chanjo
Jan 12, 2021 01:40Afisa wa ngazi za juu katika sekta ya afya nchini Iran amesema, Jamhuri ya Kiislamu ina wasi wasi kuwa taasisi muhimu za dunia kama vile Umoja wa Mataifa (UN) na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinapendelea teknolojia ya Marekani ambayo haijafanyiwa majaribio ya kutosha katika uga wa chanjo ya COVID-19 au corona.
-
Iran yataka Polisi ya Kimataifa (Interpol) iwakamate wauaji wa mashahidi Soleimani, Fakhrizadeh
Jan 12, 2021 01:36Msemaji wa Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Iran imeikabidhi Polisi ya Kimataifa, Interpol, taarifa kuhusu watu wanne waliohusika katika mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia wa Iran shahidi Mohsen Fakhrizadeh na pia watu wengine waliohusika katika mauaji ya shahidi Qassem Soleimani."
-
Khatibzadeh: Iran haiwezi kuwa mateka wa mashinikizo bandia ya watu walioshindwa
Jan 11, 2021 08:42Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran ikiwa serikali husika katika fremu ya ufundi na uchukuaji maamuzi kwa kujitegemea ndio inayopaswa kutoa majibu ya tukio la kuanguka ndege ya Ukraine katika anga ya taifa hili na kwamba, katu haitakubali kuwa mateka wa siasa na mashinikizo ya bandia ya pande zilizoshindwa.
-
Chanjo ya corona ya Iran na Cuba yapasi majaribio ya awali ya mwanadamu
Jan 11, 2021 04:36Mshauri wa Waziri wa Afya wa Iran ametangaza habari ya kufanyika kwa mafanikio hatua ya awali ya majaribio ya mwanadamu ya chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na Iran kwa kushirikiana na Cuba.
-
Karibu wagonjwa milioni 1 na laki 7 na 50,000 wapata afueni ya COVID-19 nchini Iran
Jan 10, 2021 09:47Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema kuwa, karibu wagonjwa milioni 1 na laki saba na 50 elfu wa COVID-19 wamepata afueni nchini Iran.
-
Takht Ravanchi: Marekani inatumia vikwao kujinufaisha binafsi
Jan 10, 2021 09:46Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, katika kipindi cha miaka yote hii, serikali za Marekani zimekuwa zikitumia vikwao kama silaha ya kuyashinikiza mataifa mengine na kujinufaisha binafsi.