Jan 11, 2021 08:06 UTC
  • Chanjo ya corona ya Iran na Cuba yapasi majaribio ya awali ya mwanadamu

Mshauri wa Waziri wa Afya wa Iran ametangaza habari ya kufanyika kwa mafanikio hatua ya awali ya majaribio ya mwanadamu ya chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na Iran kwa kushirikiana na Cuba.

Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo na kumnukuu Mshauri wa Waziri wa Afya,

Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Bw. Alireza Vahabzadeh akiandika jana katika mtandao wa kijamii kwamba, chanjo ya corona iliyotengenezwa na Taasisi ya Pasteur ya Iran kwa kushirikiana na Cuba, imefanikiwa vizuri katika hatua ya awali ya majaribio ya mwanadamuu na sasa hivi hatua ya pili ya majaribio hayo inafanyika nchini Cuba ili karibuni hivi iweze kuingia katika hatua yake ya mwisho.

Mshauri huyo wa Waziri wa Afya wa Iran amesisitiza kuwa, kwa juhudi za taasisi ya Pasteur, chanjo ya COVID-19 itazalishwa nchini Iran kwa ushirkiano baina yake na Cuba ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano wa huko nyuma wa nchi hizo mbili.

Mtu wa kwanza kabisa kufanyiwa majaribio ya chanjo ya corona ya Iran iitwavyo "Coviran Barekat"

 

Taasisi moja yenye historia ndefu ya uzalishaji chanjo ya Cuba kwa kushirikiana na taasisi ya Pasteur ya Iran zinaendelea na juhudi za pamoja za kuzalisha chanjo ya corona.

Kirusi cha corona kiligunduliwa mwishoni mwa mwaka 2019 katika mji wa Wuhan nchini China na baada ya muda mfupi maambukizi ya kirusi hicho yalienea dunia nzima. Mwaka 2020, Shirika la Afya Duniani WHO lililazimika kuutangaza kuwa ni mwaka wa jenga la COVID-19.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za serikali za nchi mbalimbali duniani, hadi hivi sasa watu 90,693,590 wameshakumbwa na ugonjwa wa COVID-19 kote ulimwenguni. 1,943,173 wameshafariki dunia hadi hivi sasa na 64,813,856 wameshapata afueni. Marekani ndiyo inayoongoza kwa mbali kwa idadi ya wagonjwa na vifo vya corona duniani.

Tags