May 31, 2024 02:30 UTC
  • Rais wa Cuba: Shambulio la Israel dhidi ya Rafah ni jinai kubwa dhidi ya ubinadamu

Rais wa Cuba ameulaani utawala wa Kizayuni kwa kuishambulia kwa mabomu kambi ya wakimbizi wa Kipalestina katika mji wa Rafah wa Ukanda wa Gaza, na kutaka kuchukuliwa hatua za kimataifa ili kuzima mashambulizi ya utawala huo ghasibu.

Rais Miguel Diaza-Canel ameandika kwenye ukurasa wake wa X akizungumzia shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya kambi ya wakimbizi wa Kipalestina huko Rafah kwamba, jeshi vamizi la Israel liliwachoma moto wananchi wa Palestina katika shambulio dhidi ya kambi ya wakimbizi katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Kwa upande wake, Waziri wa Mashauuri ya Kigeni wa Cuba Bruno Rodríguez amesema: "Tunalaani shambulio hili, ambalo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu. "Mauaji haya ya kikatili ya mamia ya wakimbizi ni moja ya ushahidi mkubwa kwamba Israel imetenda jinai za kivita dhidi ya watu wa Palestina.

 

Picha na video zinazoonyesha viwiliwili vilivyokatika katika na kuteketea kwa moto, baadhi yao vikiwa ni vya watoto wachanga, zimeibua vilio na hisia kali za kimataifa na kuwafanya makumi ya maelfu ya watu waingie barabarani na kuandamana katika miji ya nchi za Magharibi kulaani jinai hiyo ya Israel.

Wakati huo huo, Mtandao mkubwa zaidi wa misaada ya kibinadamu duniani umesisitizia udharura wa kusitishwa vita katika Ukanda wa Gaza, eneo ambalo mamilioni ya Wapalestina wanakabiliwa na baa la njaa.

Tags