Takht Ravanchi: Marekani inatumia vikwao kujinufaisha binafsi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65693-takht_ravanchi_marekani_inatumia_vikwao_kujinufaisha_binafsi
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, katika kipindi cha miaka yote hii, serikali za Marekani zimekuwa zikitumia vikwao kama silaha ya kuyashinikiza mataifa mengine na kujinufaisha binafsi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 10, 2021 09:46 UTC
  • Takht Ravanchi: Marekani inatumia vikwao kujinufaisha binafsi

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, katika kipindi cha miaka yote hii, serikali za Marekani zimekuwa zikitumia vikwao kama silaha ya kuyashinikiza mataifa mengine na kujinufaisha binafsi.

Majid Takht Ravanchi amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na tovuti ya Baraa la Stratijia la Uhusiano wa Mambo ya Nje kuhusu chokochoko za kijeshi za Marekani katika eneo hili na kuongeza kuwa, katika kipindi chote cha miaka ya hivi karibuni, rais wa Marekani aliyemaliza muda wake madarakani, amefanya mambo ya ajabu ajabu na kuna uwezekano katika siku zilizobakia za serikali yake, akachukua hatua nyingine zisizotabirika.

Hata hivyo amesema, ni jambo lililo mbali kuweza Donald Trump kutumia silaha za nyuklia katika siku hizi za mwisho wa uongozi wake kutokana na hali ilivyo kimataifa hivi sasa na hasa huko Marekani kwenyewe.

Rais wa Marekani, Donald Trump

 

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amezungumzia pia siasa ambazo huenda zikafuatwa na serikali ijayo nchini Marekani akifafanua kuwa, kimsingi hakuna tofauti yoyote katika siasa za mambo ya kigeni za serikali za Marekani, ziwe za Wademocrat au za Warepublican.

Mwanadiplomasia huyo wa Iran vile vile amesema, ni kweli kwamba serikali ya Trump iliendesha siasa za ajabu na zisizotabirika, kwani siasa za serikali hiyo, iwe ni kuhusu Iran au nchi nyinginezo, zilikuwa hazitabiriki na huo ndio mtazamo wa wataalamu wote wa ndani na nje ya Marekani.