Zarif: Kurejea Marekani JCPOA bila vikwazo kuondolewa si kwa maslahi ya Iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kurejea Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA bila Iran kuondolewa vikwazo ni kwa maslahi ya Marekani ni wala si kwa maslahi ya Tehran.
Zarif ameyasema hayo katika mahojiano na tovuti ya khamenei.ir na kuongeza kuwa: "Wamarekani wanamsemo usemao kuwa 'kile ambacho ni changu kitabakia kuwa changu nacho chako tunaweza kukijadili'. Zarif amesema Wamarekani wafahamu kuwa wanaweza kutumia kanuni hiyo kwa wengine lakini katu hawewezi kuitumia katika muamala na Iran, ambayo ni moja kati ya mataifa makongwe zaidi duniani.
Zarif amekumbusha kuwa 'Mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) ambayo pia ni maarufu kama mapatano ya nyuklia ya Iran si kama mlango unaozunguka ambao unaingilia upande mmoja na kutoka upande mwingine." Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuhusu kuzingatiwa kanunu za kimataifa. Huku akiashiria vikwazo vya rais Trump wa Marekani anayeondoka dhidi ya mashirika 50 ya China katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Zarif amesema washirika wetu wamepata hasara na wanapaswa kulipwa fidia.

Ameongeza kuwa, iwapo rais ajaye wa Marekani Joe Biden atasaini dikrii ya kuondolewa vikazo hilo halitatosha na muhimu zaidi ni kutekelezwa amri hiyo kivitendo.
Kuhusu uwezekano wa kuwekwa masharti mapya kabla ya vikwazo kuondolewa nchi wanachama wa mapatano ya JCPOA, Zarif amesema hawana haki ya kuchukua hatua kama hiyo.