-
Russia: Ushirikiano wetu na Iran katika masuala ya nishati ni muhimu
Dec 24, 2020 00:01Mkuu wa Kituo cha Usalama wa Nishati cha Russia amegusia safari ya Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Moscow na kusema kwamba, kustawishwa ushirikiano wa pande hizi mbili katika sekta za mafuta, gesi na vinu mbalimbali ni jambo muhimu sana. Amesema, mustakbali wa ushirikiano huo ni mzuri na uko wazi.
-
Wairani 10,000 tayari kupigwa chanjo ya majaribio ya Covid-19 iliyozalishwa nchini
Dec 23, 2020 08:57Takriban wananchi elfu kumi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wametangaza utayarifu wao wa kushiriki katika majaribio ya chanjo ya corona iliyozalishwa hapa nchini.
-
Rouhani: Hatima ya Trump haitakuwa bora kuliko ya dikteta Saddam
Dec 23, 2020 08:54Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatima ya Rais anayeondoka wa Marekani, Donald Trump haitakuwa bora kuliko ya dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein.
-
Balozi wa Iran UN: Pendekezo la aina yoyote la kufanya mazungumzo mapya kuhusu JCPOA linahalifu azimio 2231
Dec 23, 2020 00:13Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, kwa mtazamo wa Iran pendekezo la aina yoyote la kufanya mazungumzo mapya kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA halikubaliki.
-
Shamkhani: Kuondoka Marekani katika eneo ni fursa ya kupatikana amani na usalama wa kudumu
Dec 22, 2020 10:00Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema, kuondoka Marekani katika eneo la Asia Magharibi kutaandaa mazingira ya kurejeshwa amani na usalama wa kudumu.
-
Zanganeh: Iran inafanya juhudi za kuuza mafuta katika soko la kimataifa
Dec 22, 2020 04:04Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Tehran inafanya jitihada za kuuza mafuta katika soko lal kimataifa licha ya kuendelea vikwazo vya kidhulma vya Marekani dhidi ya nchi hii.
-
Zarif: Nchi za Ulaya zimekiuka wajibu wao katika JCPOA
Dec 22, 2020 00:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema data za miamala ya kibiashara baina ya nchi hii na Ulaya kati ya mwaka 2014 na 2019 zinaonesha wazi kuwa nchi tatu za Ulaya washiriki wa mapatano ya nyuklia ya JCPOA zilikiuka wajibu wao wa kisheria.
-
Khatibzadeh: Iran haitafanya mazungumzo na yoyote kuhusu usalama wa taifa
Dec 21, 2020 09:52Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina vipaumbele vyake katika masuala ya ulinzi na inchukua hatua kwa kuzingatia wa vipaumbele hivyo. Amesema: Iran imeonyesha katika muqawama wa kiwango cha juu kwamba haifanyi mazungumzo na yoyote kuhusu usalama wake wa taifa na kuhusu masuala yake muhimu.
-
Kiongozi Muadhamu: Jihadi ya wauguzi katika siku za corona imewafanya wapendwe zaidi kuliko wakati wowote ule
Dec 20, 2020 08:25Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemuelezea muuguzi kama malaika wa rehma; na akasema: Katika kipindi cha corona na katika mazingira magumu mno ya jakamoyo na wasiwasi mkubwa zaidi kuliko ya hali ya kawaida, wauguzi wameweka kumbukumbu ya kazi kubwa na wamejituma na kufanya mambo ambayo kwa kweli ni ya kustaajabisha.
-
Hakuna mazungumzo mapya yatakayofanyika kuhusu JCPOA
Dec 19, 2020 23:12Mapatano ya nyuklia ya JCPOA ni mapatano ya kimataifa yaliyofikiwa na pande kadhaa mbazo zinatakiwa kuyatekeleza kivitendo na kwa hivyo mapendekezo ya upande mmoja ya kutaka mazungumzo mapya yafanyike katika uwanja huo ni jambo lisilowezekana.