Zanganeh: Iran inafanya juhudi za kuuza mafuta katika soko la kimataifa
Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Tehran inafanya jitihada za kuuza mafuta katika soko lal kimataifa licha ya kuendelea vikwazo vya kidhulma vya Marekani dhidi ya nchi hii.
Bijan Namdar Zanganeh amesema kuwa: Hakuna mazungumzo yoyote waliyofanya kuhusu namna Iran inavyoweza kuuza mafuta yake kwa kushirikiana na Russia. Waziri wa Mafuta wa Iran alieleza hayo jana usiku pambizoni mwa mazungumzo kati yake na Aleksandr Novak Naibu Waziri Mkuu wa Russia.
Namdar Zanganeh ambaye amefanya safari huko Moscow kwa lengo la kuchunguza hali ya soko la mafuta duniani; amesema kuhusu mazungumzo yake na viongozi wa Russia kwamba: Russia katika miaka ya karibuni imekuwa na nafasi muhimu katika kuwa na uthabiti soko la mafuta duniani na katika safari yake hiyo ameshauriana na viongozi wa Russia kuhusu suala la Opec Plus; ambapo mitazamo ya pande mbili kuhusu suala hilo inakaribiana kwa kuzingatia ushirikiano wa dhati uliopo kati ya Tehran na Moscow katika soko la mafuta.