Khatibzadeh: Iran haitafanya mazungumzo na yoyote kuhusu usalama wa taifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65322-khatibzadeh_iran_haitafanya_mazungumzo_na_yoyote_kuhusu_usalama_wa_taifa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina vipaumbele vyake katika masuala ya ulinzi na inchukua hatua kwa kuzingatia wa vipaumbele hivyo. Amesema: Iran imeonyesha katika muqawama wa kiwango cha juu kwamba haifanyi mazungumzo na yoyote kuhusu usalama wake wa taifa na kuhusu masuala yake muhimu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 21, 2020 09:52 UTC
  • Khatibzadeh: Iran haitafanya mazungumzo na yoyote kuhusu usalama wa taifa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina vipaumbele vyake katika masuala ya ulinzi na inchukua hatua kwa kuzingatia wa vipaumbele hivyo. Amesema: Iran imeonyesha katika muqawama wa kiwango cha juu kwamba haifanyi mazungumzo na yoyote kuhusu usalama wake wa taifa na kuhusu masuala yake muhimu.

Akizungumza mapema leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya intaneti, Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kuwa, mapatano ya JCPOA yalijadiliwa, kusainiwa na kuidhinishwa; kwa msingi huo hakuna mtu anayeweza kudhani kwamba suala hilo linaweza kurejeshwa tena mezani na kujadiliwa upya. 

Mapatano ya JCPOA yaliyopasishwa na Baraza la Usalama la UN 

Khatibzadeh ameashiria pia kufanyika kikao kisicho rasmi cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi husika ndani ya mapatano ya JCPOA na kueleza kuwa: kikao hicho ambacho kimefanyika leo kwa njia ya intaneti hakikujadili masuala mapya ya JCPOA bali kimechunguza matukio mbalimbali ya miezi kadhaa iliyopita kuhusu mapatanoo hayo.  

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia ameeleza kuwa uhusiano wa Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki ni wa kiufundi na akaushauri wakala huo ujiweke mbali na mambo na mashinikizo ya kisiasa ili kulinda hadhi na heshima yake na vile vile ushirikiano wa kiufundi kati yake na Iran.  

Kuhusu matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada aliyedai kuwa nchi hiyo itawasilisha mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) iwapo haitaridhishwa na mwenendo wa uchunguzi na hukumu watakazopewa wale wote waliohusika na kutunguliwa ndege ya Ukraine; Khatibzadeh amesisitiza kuwa: matamshi ya uingiliaji kati ya viongozi wa Canada hayakubaliki. Amesema ripoti ya kiufundi ya tukio hilo iko tayari na itatolewa hivi karibuni.