-
Waziri wa Ulinzi wa Iraq aonana na Brigedia Jenerali Baqeri
Nov 15, 2020 04:35Waziri wa Ulinzi wa Iraq ambaye yuko ziarani hapa nchini Iran ameonana na kuzungumza na Mkuu wa Komandi Kuu ya Vikozi vya Ulinzi vya Iran.
-
Waziri wa Ulinzi: Iran iko tayari kudhamini mahitaji ya vikosi vya ulinzi vya Iraq
Nov 15, 2020 00:32Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema, Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kudhamini mahitaji ya vikosi vya ulinzi vya Iraq kwa shabaha ya kuimarisha uwezo wa kiulinzi wa nchi hiyo.
-
Watu wengine 452 wafariki dunia kwa virusi vya corona nchini Iran
Nov 14, 2020 08:40Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema kuwa, watu wengine zaidi elfu 11 wameambukizwa virusi vya corona na wengine 452 wamefariki dunia katika muda wa saa 24 zilizopita.
-
Iran yapuuzilia mbali madai ya kuuawa kinara wa al-Qaeda hapa nchini
Nov 14, 2020 04:48Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu Iran amekanusha vikali habari za kipropaganda zinazodai kuwa kiongozi wa ngazi za juu wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda ameuawa hapa nchini.
-
Iran yaishauri Saudia iache kujipendekeza kwa Israel
Nov 14, 2020 03:48Msaidizi maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa ameiasa Saudi Arabia ikomeshe mienendo yake ya kujipendekeza, kujidhalilisha na kujikomba kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Chanjo 5 za COVID-19 za Iran zinasubiri kupasishwa na WHO
Nov 13, 2020 23:04Msemaji wa Shirika la Chakula na Madawa la Iran ametangaza kuwa, chanjo 5 za corona zilizotengenezwa nchini Iran, hivi sasa zinasubiri kupasishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
-
Watu 546,000 wamepona corona Iran hadi sasa
Nov 13, 2020 08:08Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Afya ya Iran Daktari Sima Sadat Lari ametangaza leo kuwa, hadi sasa watu 738,000 wameambukizwa corona au COVID-19 nchini na kuwa miognoni mwao 546,642 wamepona.
-
Naibu Waziri wa Afya: Chanjo ya corona ya Iran iko kwenye awamu ya utengenezaji
Nov 13, 2020 04:34Naibu Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran anayehusika na teknolojia na utafiti amesema, chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 iliyobuniwa hapa nchini iko kwenye awamu ya utengenezaji.
-
Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Iran, muendelezo wa njama za aliyeshindwa
Nov 12, 2020 07:13Baada ya Donald Trump kuitoa Marekani katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia yajulikanayo kwa jina la JCPOA hapo mwezi Mei 2018, Washington iliiwekea Iran vikwazo vya kiwango cha juu na hadi leo hii, kila siku inaweka vikwazo vipya.
-
Rais Rouhani: Mashinikizo ya kiwango cha juu yanaelekea ukingoni
Nov 12, 2020 07:08Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani yanaelekea ukingoni na kuongeza kuwa, taifa la Iran hivi karibuni litavuna matunda ya kusimama kwake kidete na imara mbele ya mashinikizo hayo.