-
Maqarii wa Qurani wa Ulimwengu wa Kiislamu walaani kuvunjiwa heshima Mtume SAW
Sep 11, 2020 03:12Maqarii mashuhuri wa Qurani Tukufu kutoka kona mbalimbali za dunia wamekutana mjini Mashhad, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambapo kwa kauli moja, wamelaani vikali hatua ya jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo ya kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad SAW.
-
Wananchi wa Iran washiriki duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge
Sep 11, 2020 02:38Wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameelekea katika masanduku ya kupigia kura kushiriki duru ya pili ya uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran).
-
Rais Rouhani: Waislamu wasimame kidete kutetea na kulinda thamani za Uislamu
Sep 11, 2020 00:16Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kulaani kitendo cha jarida la Charlie Hebdo la Ufaransa cha kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW, ameyataka mataifa ya Kiislamu kusimama kidete kutetea na kulinda thamani, utamaduni na matukufu ya dini yao.
-
Iran: Uingereza ichukue hatua za kivitendo kutulipa mamia ya mamilioni ya fedha zetu
Sep 11, 2020 00:14Wizara ya Ulinzi ya Iran imeashiria jinsi Uingereza ilivyokiri kuwa ina deni la miaka 40 la Iran na kuitaka London ichukue hatua za kivitendo za kuilipa Tehran fedha zake hizo ambazo ni mamia ya mamilioni.
-
Mazoezi ya kijeshi ya Dhulfiqar-99 na azma ya kuimarisha amani na usalama
Sep 11, 2020 00:13Vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimeanza mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la maji ya mashariki mwa Lango Bahari la Hormuz, pwani ya Makran, Bahari ya Oman na kaskazini mwa Bahari ya Hindi.
-
Iran nzima yaandamana kulaani vikali kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW nchini Ufaransa
Sep 10, 2020 07:31Wananchi wa Iran wameendelea kuandamana kulaani kwa nguvu zao zote ufidhuli wa jarida ya Charlie Hebdo la Ufaransa wa kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na pia kitendo cha maadui wa Uslamu cha kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu katika mji wa Malmö wa kusini mwa Sweden.
-
Iran yafanyia majaribio kwa mafanikio kombora lake jipya
Sep 10, 2020 07:09Kombora lililoboreshwa na kuongezewa nguvu la Shalamcheh la kikosi cha ulinzi wa anga cha jeshi la Iran limefanyiwa majaribio kwa mafanikio katika maneva ya "Dhulfiqar 99."
-
Wakazi wa Qum, Iran, waandamana wakipinga kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad (saw)
Sep 10, 2020 03:17Wakazi na wanafunzi wa vyuo vya mji wa Qum ulioko umbali wa karibu kilomika 160 kusini mwa jiji la Tehran wamefanya maandamano makubwa wakilaani hatua ya jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo ya kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
-
Rais Rouhani: Marekani kamwe haitofikia malengo yake dhidi ya Iran
Sep 09, 2020 07:16Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia hatua za kiuadui zinazochukuliwa na Marekani kama vikwazo vyake vya kidhalimu dhidi ya taifa la Iran na kusema kuwa, viongozi wa Washington kamwe hawatofikia malengo yao haramu.
-
Zaidi ya wagonjwa laki tatu na 39 elfu wapata afueni ya corona nchini Iran
Sep 09, 2020 07:13Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa, wagonjwa waliopata afueni ya ugonjwa wa COVID-19 hapa nchini imepindukia watu 339,000.