Iran yafanyia majaribio kwa mafanikio kombora lake jipya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63338-iran_yafanyia_majaribio_kwa_mafanikio_kombora_lake_jipya
Kombora lililoboreshwa na kuongezewa nguvu la Shalamcheh la kikosi cha ulinzi wa anga cha jeshi la Iran limefanyiwa majaribio kwa mafanikio katika maneva ya "Dhulfiqar 99."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 10, 2020 07:09 UTC
  • Iran yafanyia majaribio kwa mafanikio kombora lake jipya

Kombora lililoboreshwa na kuongezewa nguvu la Shalamcheh la kikosi cha ulinzi wa anga cha jeshi la Iran limefanyiwa majaribio kwa mafanikio katika maneva ya "Dhulfiqar 99."

Hatua kuu na ya asili ya luteka na maneva ya pamoja ya "Dhulfiqar 99" ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yameanza leo Alkhamisi asubuhi kwa kauli ya "Yaa Sayyidash Shuhadaa AS" na kwa kaulimbiu ya "Amani ya Kudumu katika Kivuli cha Nguvu za Kiulinzi." Maneva hayo yanafanyika kusini mwa Iran.

Idara ya Mawasiliano ya Uma ya Jeshi la Iran imetoa ufafanuzi zaidi kwa kusema, wakati wa mazoezi hayo ya kijeshi, ndege "adui" amejaribu kuingia katika eneo hilo akiwa anaruka kwa kasi kubwa na kwenye masafa ya juu sana, ndege huyo ameonekana kwa tabu katika rada, hata hivyo mfumo wa kujilinda na mashambulizi ya anga unaoongozwa na kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatamul Anbiyaa umekigundua chombo hicho na kutumia haraka kombora la Shalamcheh lililoboreshwa na kumtungua bila kuchelewa ndege huyo "adui."

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nguvu kubwa za makombora zinazowatia kiwewe maadui

 

Admerali Shahram Irani, Msemaji wa Maneva ya "Dhulfiqar 99" amegusia uwezo mkubwa wa makombora yaliyotengenezwa na wataalamu wenye wa Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya adui na kuongeza kuwa, kutoruhusu aina yoyote ya kujipenyeza adui katika nchi ya Iran na kuweza kuongoza mifumo ya kulinda kwa makombora kutoka aneo lolote lile ni miongoni mwa mafanikio yaliyooneshwa kwenye luteka hiyo ya "Dhulfiqar 99."