Iran nzima yaandamana kulaani vikali kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW nchini Ufaransa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63341-iran_nzima_yaandamana_kulaani_vikali_kuvunjiwa_heshima_mtume_muhammad_saw_nchini_ufaransa
Wananchi wa Iran wameendelea kuandamana kulaani kwa nguvu zao zote ufidhuli wa jarida ya Charlie Hebdo la Ufaransa wa kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na pia kitendo cha maadui wa Uslamu cha kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu katika mji wa Malmö wa kusini mwa Sweden.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 10, 2020 07:31 UTC
  • Iran nzima yaandamana kulaani vikali kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW nchini Ufaransa

Wananchi wa Iran wameendelea kuandamana kulaani kwa nguvu zao zote ufidhuli wa jarida ya Charlie Hebdo la Ufaransa wa kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na pia kitendo cha maadui wa Uslamu cha kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu katika mji wa Malmö wa kusini mwa Sweden.

Leo Alkhamisi, wananchi wa Iran katika kona zote za nchi wameandamana kuonesha kukasirishwa mno na vitendo hivyo viovu na ufidhuli huo wa maadui wa Uislamu barani Ulaya na kusema kuwa, kitendo cha wananchi wa Ufaransa cha kudharau jinai hiyo na kunyamazia kimya ufidhuli huo, kinapaswa kulaaniwa.

Wananchi wa Iran walioshiriki kwenye maandamano hayo katika kona zote za Iran wametoa tamko la pamoja na kulaani vitendo vyote vya chuki na vya kiuadui dhidi ya matukufu ya mabilioni ya watu huru duniani na kusema kuwa vitendo hivyo vinatokana na siasa za kiuadui na njama za Marekani na utawala pandikizi wa Kizayuni unaoua watoto wadogo wasio na hatia huko Palestina.

Waislamu Iran hata wakati wa corona, wamefanya maandamano kulaani kuvuniwa heshima Mtume Muhammad SAW huko Ufaransa

 

Waandamanaji hao aidha wamelaani usaliti usiosameheka wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) wa kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni kama ambavyo wamezionya pia nchi nyingine vibaraka za Kiarabu ambazo zimo kwenye mkumbo huo wa kutaka kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala huo pandikizi.

Wananchi hao wa Iran wamezitaka jamii za kimataifa na wapenda haki na Waislamu wote duniani kuwa na kauli moja ya kukabiliana na maadui wanaovunjia heshima mtukufu ya Uislamu ambao wanafanya ufidhuli dhidi ya Bwana Mtume Muhammad SAW na Kitabu Kitakatifu cha Qur'ani.