-
Kuendelea kutumiwa haki za binadamu na madola ya Magharibi kama wenzo wa kufikia malengo ya kisiasa
Nov 19, 2019 09:03Kamati ya Haki za Binadamu ya Idara ya Mahakama ya Iran imelaani hatua ya serikali ya Canada ya kuwasilisha rasimu ya azimio yenye anuani isemayo "Hali ya Haki za Binadamu nchini Iran" na kutangaza kuwa, rasimu hiyo imejaa uongo, uzishi na taarifa zisizo sahihi na ni mwendelezo wa chuki za serikali ya Ottawa dhidi ya Tehran.
-
"Ni fedheha kwa Marekani kuwaunga mkono Wairani wanaofanya fujo"
Nov 19, 2019 04:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ni fedheha kwa Marekani kutangaza wazi wazi kuwa inawaunga mkono wanaofanya fujo na kuzusha ghasia kwa kisingizio cha kulalamikia ongezeko la bei ya petroli hapa nchini.
-
IAEA yathibitisha; akiba ya maji mazito ya Iran ni zaidi ya tani 130
Nov 19, 2019 04:30Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA umethibitisha kuwa akiba ya maji mazito kwenye kinu cha maji mazito cha Arak kilichoko mkoa wa Markazi nchini Iran ni zaidi ya tani 130.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kuhusu udharura wa kutekeleza maamuzi ya wakuu wa nchi na ulazima wa kuwa macho mbele ya wanaotaka kuvuruga utulivu na amani katika jamii
Nov 19, 2019 02:25Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya miji ya Iran imeshuhudia ukosefu wa usalama kufuatia uamuzi wa viongozi wa mihimili mitatu ya dola kutekeleza mpango wa usimamizi bora wa mafuta ya petroli. Matukio hayo chungu ambayo yaliandamana na ghasia na utumiaji mabavu na hivyo kupelekea kuharibiwa au kuteketezwa baadhi ya maeneo ya umma pia yamepelekea watu kadhaa ya kupoteza maisha.
-
Zarif azungumza na Haniya, asema Iran imesimama pamoja na taifa la Palestina
Nov 19, 2019 01:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif amefanya mazungumzo na Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, na kumpongeza kufuatia ushindi wa wanamuqawama (wanamapambano) wa Palestina mbele ya utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko pamoja na taifa la Palestina na inasimama pamoja na wanamapambano shujaa katika Ukanda wa Ghaza."
-
Raisi: Wamagharibi wanaowaunga mkono wafanya fujo nchini Iran hawajui uimara wa Jamhuri ya Kiislamu
Nov 18, 2019 23:11Mkuu wa Chombo cha Mahakama cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Wamagharibi na vibaraka wao wanaowaunga mkono wahalifu wanaofanya fujo na kuharibu mali za umma humu nchini, ni watu ambao wanafanya uchochezi wakiwa nje ya mipaka ya Iran na hawatambui uimara wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
"Marekani inakusudia kuteka nyara maandamano ya amani ya Wairani"
Nov 18, 2019 08:44Msemaji wa serikali ya Iran amesema Marekani inafanya juu chini ili kupotosha mkondo wa maandamano ya amani ya wananchi wa Iran wanaolalamikia ongezeko la bei ya petroli, lakini njama hizo zitagonga mwamba.
-
Rouhani: Wairani wana haki ya kuandamana bila kufanya fujo
Nov 18, 2019 08:14Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema wananchi wa taifa hili wana haki ya kufanya maandamano, lakini maandamano ya amani ni tofauti na uibuaji wa fujo na hali ya mchafukoge.
-
Larijani: Marekani imekusudia kutoa pigo kwa wananchi wa Iran
Nov 18, 2019 04:02Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ameashiria matasmhi ya uingiliaji ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ya kuunga mkono fujo na uharibifu wa kuchomwa mali za umma nchini Iran na kueleza kuwa: Viongozi wa Marekani wameazimia kutoa pigo kwa wananchi wa Iran.
-
Iran yajibu matamshi ya kichochezi ya Pompeo
Nov 18, 2019 00:02Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekemea msimamo wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo wa kuliunga mkono kundi dogo la watu waliohusika na machafuko katika miji kadhaa hapa nchini na kusema: Hatua za baadhi ya watu waharibifu na wanaozusha fujo wanaoungwa mkono na mithili ya Mike Pompeo hazioani na mwenendo wa wananchi wengi wa Iran wenye utambuzi na muono wa mbali.