-
Azimio la maadhimisho ya tarehe 13 Aban; sisitizo la wananchi wa Iran la kuendeleza muqawama
Nov 04, 2019 08:46Washiriki katika marasimu ya maadhimisho ya tarehe 13 Aban kote nchini Iran wamesisitiza katika azimio lililotolewa mwishoni mwa maandamano hayo kuwa: Stratejia ya muqawama ulio hai mkabala na njama za Marekani na waitifaki wake ni jukumu la kidini na lengo lisilobadilika la Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Bunge la Iran larindima nara na kaulimbiu za "Mauti kwa Marekani" na "Mauti kwa Israel"
Nov 04, 2019 04:34Sambamba na maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari Duniani yanayofanyika kote nchini hii leo, wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran wametoa nara za "Mauti kwa Marekani" na "Mauti kwa Israel" katika ufunguzi wa kikao cha leo cha bunge.
-
Watu wasiojulikana washambulia ubalozi mdogo wa Iran katika mji wa Karbala, Iraq
Nov 04, 2019 04:14Kanali ya televisheni ya Al-Alam imeripoti kuwa watu wasiojulikana wameshambulia ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mji wa Karbala katikati mwa Iraq.
-
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu mkesha wa Siku ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa
Nov 04, 2019 03:36Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei jana Jumapili alihutubia hadhara kubwa ya melfu ya wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya Iran katika mkesha wa maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa akisisitiza kuwa mapinduzi ya tarehe 28 Mordad (mwezi Agosti mwaka 1953) yalikuwa mwanzo wa uadui wa waziwazi wa Shetani Mkubwa dhidi ya taifa la Iran.
-
Raisi: Marekani ifunguliwe mashtaka kutokana na jinai zilizofanywa na Daesh
Nov 03, 2019 23:43Mkuu wa Idara ya Mahakama za Iran amesema kuwa, Wamarekani wamekiri rasmi kwamba ndio walioanzisha kundi la kigaidi la Daesh, kwa msingi huo wanapaswa kufunguliwa mashtaka kutokana na jinai zilizofanywa na kundi hilo.
-
Raisi: Marekani ifikishwe kizimbani kwa kuasisi kundi la kigaidi la ISIS
Nov 03, 2019 09:05Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Marekani imekiri rasmi kuwa ilianzisha kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) na kwa msingi huo inapaswa kufikishwa kizimbani kujibu mashtaka kuhusu jinai za kundi hilo."
-
Kiongozi Muadhamu: Mazungumzo na Marekani hayajakuwa na matokeo yoyote
Nov 03, 2019 08:59Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mazungumzo na Marekani hayajakuwa na matokeo yoyote na kusisitiza kuwa: "Mazungumzo na Marekani hayajakuwa na faida kwa sababu hawataki kulegeza msimamo hata kidogo."
-
Larijani: Trump ni nembo ya sura ya kuogofya ya Marekani
Nov 03, 2019 04:31Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema tabia ya Donald Trump ya kufichua sera haribifu zilizofichika za Ikulu ya White House ya Marekani imeweka hadharani sura halisi, mbaya na ya kuogofya ya Washington.
-
Abbas Mousavi: Vikwazo vya kukaririwa vya Marekani havitaifikisha popote Washington
Nov 02, 2019 23:05Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Tehran na kusema kuwa, vikwazo vya kukaririwa vya Washington havitalifikisha katika malengo yake taifa hilo la Magharibi.
-
SEPAH: Watu milioni 8.5 wameuawa kutokana na uingiliaji mambo wa Marekani
Nov 02, 2019 09:13Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema watu zaidi ya milioni nane na laki tano wameuawa kutokana na uingiliaji wa mambo wa Marekani wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja katika eneo na katika ulimwengu wa Kiislamu, ndani ya miaka 40 iliyopita.