-
Salami: Stratijia ya muqawama imepelekea adui akose irada
Sep 30, 2019 23:18Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema stratijia ya muqawama au mapambano ya Kiislamu imepelekea adui adorore na akose irada. Ameongeza kuwa, hivi sasa maadui wameanza kudidimia kwa namna ambayo hawawezi kupata nguvu tena na hifadhi zao za kistratijia zinaelekea kumalizika.
-
Iran: Nchi za eneo zijue kwamba usalama si kitu cha kununua
Sep 30, 2019 10:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, Jamhuri ya Kiislamu inataka usalama wa Ghuba ya Uajemi uletwe na nchi zenyewe za eneo na akasisitiza kuwa: Nchi za eneo zielewe kwamba usalama si kitu cha kununua.
-
Ushirikiano na nchi za Mashariki ya Kati; stratijia ya Iran ya kulinda usalama wa safari za baharini Ghuba ya Uajemi
Sep 30, 2019 04:07Hossein Dehghani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika Masuala ya Sheria na Kimataifa amesema katika kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC pambizoni mwa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York Marekani kwamba, mizozo ya aina yoyote ni hatari kwa eneo hili zima.
-
Zarif aikosoa Ulaya kwa kufuata mdundo wa ngoma ya Trump
Sep 30, 2019 04:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali nchi za Ulaya hususan Ujerumani, Ufaransa na Uingereza ambazo zilisaini makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, kwa kushangilia madai na kauli zisizo na msingi zinazotolewa na Marekani dhidi ya Iran.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Uchokozi wowote wa adui utapata jibu kali
Sep 29, 2019 23:48Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema chokochoko yoyote ya adui itapokea jibu kali kutoka kwa vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu.
-
JCPOA haina maana iwapo haiwafaidi na chochote wananchi wa Iran
Sep 29, 2019 23:06Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hayana faida yoyote iwapo wananchi wa Iran hawastafidi chochote kutokana na mapatano hayo ya kimataifa.
-
Admeri Alireza Tangsiri: Kikosi cha wanamaji wa SEPAH kimejiandaa kulinda mipaka ya majini ya Iran
Sep 29, 2019 09:07Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, chokochoko yoyote ile dhidi ya mipaka ya majini ya Iran itakuwa na matokeo mabaya na machungu kwa wavamizi.
-
Iran yazindua dawa sita mpya
Sep 29, 2019 04:02Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua dawa sita mpya ikiwa ni katika jitihada za kujitosheleza katika sekta ya uzalishaji dawa nchini.
-
Zarif: Iwapo Marekani inataka mazungumzo na Iran lazima itekeleze ahadi zake
Sep 29, 2019 03:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran haitaacha mustakabali wa uchumi na wananchi wake utegemee mkutano wa kimaonyesho na Rais Donald Trump wa Marekani. Ameongeza kuwa, kama ambavyo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alivyosema, 'iwapo Mareknai inataka kufanya mazungumzo na Iran, ni lazima kwanza itekeleze ahadi zake na isitishe vikwazo.'
-
Brigedia Jenerali Nilforooshan: Israel imezungukwa na Iran kila upande
Sep 28, 2019 08:53Kamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema utawala wa Kizayuni wa Israel umezingirwa kila upande na Iran na kuuonya utawala huo haramu dhidi ya kuchukua hatua yoyote ya kichokozi dhidi ya taifa hili.