-
Ombi la Shirika la Haki za Binadamu la Ulaya-Mediterranean la kuwekewa vikwazo Israel
Aug 22, 2024 07:16Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Ulaya na Mediterania (The Euro-Mediterranean Human Rights Monitor-Euro-Med-) limeonya katika taarifa yake siku ya Jumatano kuhusu amri za mara kwa mara za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuwataka Wapalestina wahame katika maeneo tofauti ya Gaza na kuzitaka nchi za dunia ziuwekee vikwazo utawala huo ghasibu na zisiuunge mkono.
-
Manowari za Marekani zawasili Asia Magharibi huku kukiwa na wasiwasi wa Iran na Hizbullah kuishambulia Israeli
Aug 22, 2024 04:18Meli ya Marekani ya kubeba ndege za kivita ya Abraham Lincoln na meli nyingine za kivita zinazoandamana nayo zimewasili katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) huku nchi hiyo na utawala haramu wa Israel zikiwa na hofu kubwa ya kushambuliwa utawala huo na Iran pamoja na Hizbullah ya Lebanon ikiwa ni katika kutoa jibu kali kwa mauaji ya kigaidi yaliyofanywa hivi karibuni na utawala wa Tel Aviv dhidi ya shakhsia waandamizi wa muqawama.
-
84% ya Misikiti ya Gaza imeharibiwa na mabomu ya Wazayuni
Aug 21, 2024 23:36Asilimia 84 ya Misikiti katika Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu imeharibiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Wanamuqawama wanne wa Hizbullah wauawa shahidi kusini mwa Lebanon
Aug 21, 2024 22:49Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon jana Jumatano ilitangaza habari ya kuuliwa shahidi wapiganaji wake wanne kusini mwa nchi hiyo.
-
Makadirio ya zaidi ya dola bilioni 80 za mashambulio ya utawala wa Kizayuni Gaza
Aug 21, 2024 22:47Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kutokana na mashambulizi ya kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, ukarabati na ujenzi mpya wa ukanda huo utagharimu zaidi ya dola bilioni 80 na mchakato huo kuchukua miongo minane kukamilika.
-
Israel yaendeleza ukatili, yaua Wapalestina 50 ndani ya saa 24 Gaza
Aug 21, 2024 08:21Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza imesema Wapalestina wasiopungua 50 wameuawa shahidi na wengine 124 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya maeneo mbali mbali ya Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita.
-
Sauti unayozidi kupaza Umoja wa Mataifa kulalamikia jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina
Aug 21, 2024 05:47Umoja wa Mataifa umeendeleza msimamo wake wa kulalamikia jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina kwa kutangaza kuwa, umetiwa na wasiwasi na uamuzi wa hivi karibuni uliotangazwa na Israel wa kupanua vitongoji vya walowezi na kubadilisha hali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Mchambuzi: Nasrullah amedhoofisha uwezo wa kujihami wa Israel
Aug 20, 2024 23:28Mtafiti mmoja wa Kizayuni amekiri uwezo wa Katibu Mkuu wa Hakarati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah na kusisitiza kuwa, kiongozi huyo wa Muqawama wa Lebanon amedhoofisha uwezo wa kuzuia mashambulizi wa utawala wa Kizayuni.
-
Wazayuni washambulia tena shule na kuua makumi ya watu Gaza
Aug 20, 2024 23:28Mashambulizi ya Israel dhidi ya Shule ya Mustafa Hafez inayohifadhi wakimbizi wa Kipalestina magharibi mwa Ukanda wa Gaza yameua takriban raia 20 na kujeruhi wengine wengi.
-
Mwakilishi wa Israel atoa wito wa kutenguliwa Umoja wa Mataifa
Aug 20, 2024 23:27Katika taarifa ya kushangaza, balozi wa utawala haramu wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Gilad Erdan, ametoa wito wa kuvunjwa kikamilifu Umoja wa Mataifa.