Wanamuqawama wanne wa Hizbullah wauawa shahidi kusini mwa Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i115494-wanamuqawama_wanne_wa_hizbullah_wauawa_shahidi_kusini_mwa_lebanon
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon jana Jumatano ilitangaza habari ya kuuliwa shahidi wapiganaji wake wanne kusini mwa nchi hiyo.
(last modified 2024-08-21T22:49:25+00:00 )
Aug 21, 2024 22:49 UTC
  • Wanamuqawama wanne wa Hizbullah wauawa shahidi kusini mwa Lebanon

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon jana Jumatano ilitangaza habari ya kuuliwa shahidi wapiganaji wake wanne kusini mwa nchi hiyo.

Harakati ya Hizbullah jana ilitoa taarifa na kutangaza kuwa, wanamuqawama wake wanne kwa majina ya Raed Ali Khattab (Mahdi), Ali Ahmad Daqmaq (Yusuf Naji) kutoka mji wa al Nabatiya na Muhammad Ghazi Shahin( Ali Ali) kutoka mji wa Sur wameuawa shahidi kusini mwa Lebanon. 

Mara baada ya makundi ya mapambano ya Palestina kutekeleza oparesheni ya Kimbunga cha al Aqsa, harakati ya Hizbullah ya Lebanon pia kila siku inatekeleza oparesheni kubwa dhidi ya maeneo mbalimbali ya utawala wa Kizayuni ndani ya ardhi ya Palestina ili kuwashughulisha wanajeshi wa Kizayuni huko kaskazini mwa Palestina na kupunguza mashinikizo kwa wanamapambano wa Gaza.  

Wanamuqawama wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon 

Kuhusiana na suala hilo, vyombo vya habari vya Israel vimekiri mara kwa mara kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon ina nguvu kubwa kubwa huko kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, na kwamba jeshi bandia la Israel limenasa katika mtego wa askari wa Hizbullah  katika eneo hilo.