Mwakilishi wa Israel atoa wito wa kutenguliwa Umoja wa Mataifa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i115454-mwakilishi_wa_israel_atoa_wito_wa_kutenguliwa_umoja_wa_mataifa
Katika taarifa ya kushangaza, balozi wa utawala haramu wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Gilad Erdan, ametoa wito wa kuvunjwa kikamilifu Umoja wa Mataifa.
(last modified 2024-08-20T23:27:32+00:00 )
Aug 20, 2024 23:27 UTC
  • Mwakilishi wa Israel atoa wito wa kutenguliwa Umoja wa Mataifa

Katika taarifa ya kushangaza, balozi wa utawala haramu wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Gilad Erdan, ametoa wito wa kuvunjwa kikamilifu Umoja wa Mataifa.

Matamshi hayo yametolewa wakati wa mahojiano na mtandao wa televisheni wa Kizayuni wa i24 News, ambapo Erdan amedai kwamba shirika hilo la kimataifa halitekelezi tena majukumu yake ya msingi duniani.

Erdan amesema, "Milango ya jengo la Umoja wa Mataifa huko New York inapaswa kufungwa, na taasisi hii inapaswa kufutwa kabisa kwenye ramani."

Balozi huyo wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Umoja wa Mataifa amedai kuwa, Umoja wa Mataifa umepotoka na kwenda mbali na malengo yake wa asili.

Hii si mara ya kwanza kwa Erdan kutoa matamshi ya kichochezi. Mwezi Mei mwaka huu 2024 wakati wa mjadala wa azimio la kupewa uanachama kamili wa Palestina katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Erdan alichana Mkataba wa UN, kitendo ambacho kiliwashangaza sana wengi na kutajwa kuwa cha kikaidi.

Utawala pandikizi wa Israel umekuwa ukikabiliwa na malalamiko makubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa kutokana na vitendo vyake vya kikatili katika Ukanda wa Gaza.

Operesheni za kijeshi za hivi karibuni za utawala huo ghasibu zimelaaniwa vikali, huku taasisi nyingi za kimataifa, ukiwemo Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, zikianzisha hatua za kisheria dhidi ya maafisa wa Israel kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.