-
Saudia yakanusha kuhusika na shambulio la Israel Hudaydah; Iran yalaani
Jul 21, 2024 03:20Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imekadhibisha ripoti za vyombo vya habari vya Israel kuwa Riyadh imeshiriki katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya mji wa al-Hudaydah, magharibi mwa Yemen.
-
Mufti wa Oman: Kuiunga mkono Yemen ni wajibu wa kila Muislamu
Jul 21, 2024 03:19Mufti Mkuu wa Oman amelaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuushambulia mji wa magharibi mwa Yemen wa al-Hudaydah, huku akiwataka Waislamu kote ulimwenguni kuliunga mkono na kulisaidia kwa hali na mali taifa hilo la Kiarabu linalosumbuliwa na ukata na umaskini mkubwa.
-
Yemen: Tuko tayari kwa vita vya muda mrefu na Israel, ni baada ya Israel kushambulia al-Hudaydah
Jul 20, 2024 23:35Vikosi vya Jeshi la Yemen vimeapa kuendeleza operesheni zinazoiunga mkono Palestina baada ya utawala haramu wa Israel kushambulia maeneo ya raia katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Mzayuni: Baada ya Yemen kushambulia Tel-Aviv, anga ya "Israel" si salama tena
Jul 20, 2024 23:04Kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa jeshi la utawala wa Kizayuni amekiri kwamba jeshi la Israel limeshindwa vibaya katika kukabiliana na droni ya Yemen iliyopiga Tel Aviv na kusisitiza kuwa, kuanzia sasa anga yote ya "Israel" si salama tena; na eneo lolote la utawala wa Kizayuni linaweza kushambuliwa bila ya kuwa na nguvu za kujikinga.
-
Msemaji wa jeshi la Yemen: Katu Ukanda wa Gaza hautakuwa peke yake
Jul 20, 2024 09:35Msemaji wa jeshi la Yemen amesema: Gaza haijawahi kuwa peke yake, ina washirika kutoka taifa kubwa ambalo ni tiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
-
Bunge la Kiarabu: Uamuzi wa Mahakama ya Haki ni ushindi kwa haki za Wapalestina
Jul 20, 2024 07:41Bunge la Kiarabu na nchi za Kiarabu zikiwemo Iraq, Misri, Jordan na Kuwait zimekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kuvitaja vitongoji ya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kuwa ni kinyume cha sheria.Taarifa ya mataifa hayo imeeleza kuwa, uamuzi wa mahakama ya ICJ ni ushindi kwa uadilifu na haki za Wapalestina.
-
Riyadh yaipongeza ICJ kuvitaja vitongoji vya Wazayuni kuwa haramu
Jul 20, 2024 04:24Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kuvitaja vitongoji ya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kuwa ni kinyume cha sheria.
-
Wapalestina wapongeza uamuzi wa ICJ dhidi ya Israel
Jul 20, 2024 02:52Makundi ya kisiasa na kijamii ya Palestina yamepongeza uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kutazama ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuwa haramu na kinyume cha sheria.
-
Mtaalamu wa kijeshi: Shambulizi la al Huothi mjini Tel Aviv linaiweka Israel katika mtanziko
Jul 19, 2024 22:50Mtaalamu wa masuala ya kijeshi na kimkakati, Meja Jenerali Mohammed Al-Samadi, amesema kuwa shambulizi la kundi la Ansarullah la Yemen katikati mwa mji wa Tel Aviv kwa kutumia ndege isiyo na rubani ni miongoni mwa operesheni hatari zaidi zilizoikabili Israel tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana.
-
Kufeli njama za kuleta fitna baina ya Waislamu nchini Afghanistan
Jul 19, 2024 22:48Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan ametangaza kuwa, katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, kumefanyika njama nyingi za kuzusha fitna baina ya Waislamu wa Kisuni na Kishia nchini humo lakini zote zimefeli.