Jun 28, 2024 07:18 UTC
  • Shirika la UNRWA laonya kuhusu uhaba wa bidhaa za chakula Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limeonya kuhusiana na uhaba mkubwa wa bidhaa za chakula unaolikabili eneo la Ukanda wa Gaza, Palestina.

Taarifa ya UNRWA imetahadharisha kwamba, hali ya uhaba wa bidhaa za chakula iinazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNWRA) limetangaza kwamba, wakaazi wa Gaza wanakumbwa na janga la njaa na watoto wanakufa kutokana na utapiamlo na kiu.

Wakati huo huo, ofisi ya habari ya serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza pia imetangaza kuwa, watoto 3,500 walio chini ya umri wa miaka 5 wanakabiliwa na kifo kutokana na utapiamlo na siasa za kudumisha njaa zinazotumiwa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wakaazi wa eneo.

 

Katika upande mwingine, shirika linalofuatilia viwango vya njaa duniani, IPC limesema Ukanda wa Gaza unaendelea kukumbwa na hatari kubwa ya njaa, wakati ambapo utawala haramu wa Israel unaendelea kufanya hujuma na mashambulio yake ya kinyama.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetoa indhari kwamba, ikiwa misaada ya kibinadamu haitaingizwa Ghaza, hakutakuwa na chakula chochote cha kuwagaia wakazi wa eneo hilo lililowekewa mzingiro.

Wakati huohuo, kutokana na kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa: tangu tarehe 7 Oktoba 2023 hadi sasa, karibu Wapalestina wasiopungua 37,000 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na utawala huo.

Tags