-
Yemen yasambaza video ya kushambulia meli ya Israel kwa kombora la 'balestiki la hypersonic'
Jun 27, 2024 04:03Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen vimesambaza video inayoonyesha kutumiwa kombora la balestiki la hypersonic dhidi ya meli ya Israeli katika Bahari ya Arabia. Vikosi hivyo vilisambaza video hiyo siku ya Jumatano, vikisema kombora lililotumika linaitwa "Hatem-2" na kwamba meli iliyolengwa ni "MSC SARAH V."
-
Kutoweka watoto katika Ukanda wa Gaza
Jun 26, 2024 22:59Kwa mujibu wa ripoti mpya zilizochapishwa na shirika la kimataifa linaloitwa "Save the Children", watoto wapatao elfu 21 wa Kipalestina wametoweka huko Ukanda wa Gaza, ambapo watoto elfu 17 wametenganishwa na familia zao kutokana na vurugu zilizosababishwa na vita, hasa operesheni za hivi karibuni za utawala wa Kizayuni katika ukanda huo.
-
Ripoti: Gaza inakabiliwa na hatari kubwa ya njaa
Jun 26, 2024 03:53Eneo la Ukanda wa Gaza linakabiliwa na hatari kubwa ya baa la njaa ikiwa ni matokeo ya hujuma na mashambulio ya kinyama ya utawala ghasibu wa Israel.
-
Muqawama Iraq: Tutashambulia maslahi ya US iwapo Lebanon itavamiwa
Jun 25, 2024 22:48Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya nchini Iraq ameuonya vikali utawala haramu wa Israel dhidi ya kuingia kwenye vita vipya na Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
-
Kuendelea mivutano kati ya Netanyahu na jeshi la Kizayuni
Jun 25, 2024 08:51Vita vya Gaza vimeingia katika mwezi wa tisa huku mizozo na mivutano kati ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na maafisa wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni ikiendelea kushika kasi.
-
Dadake Haniya ni miongoni mwa makumi waliouawa na mabomu ya Israel Gaza
Jun 25, 2024 08:00Dada yake Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ni miongoni mwa makumi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi mapya ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel katika pembe mbali mbali za Ukanda wa Gaza.
-
Njaa yaenea Gaza kutokana na kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni
Jun 25, 2024 04:14Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa njaa inazidi kuongezeka katika keneo kila siku kufuatia kushtadi mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa ukanda huo.
-
Ripoti: Mayatima wameongezeka Gaza baada ya Israel kuanzisha hujuma ya kijeshi
Jun 24, 2024 22:59Ofisi ya vyombo vya habari ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina huko Gaza imetangaza ongezeko la maelfu ya watoto mayatima tangu kuanza kwa mashambulizi ya Wazayuni katika Ukanda wa Gaza Oktoba mwaka jana (2023).
-
Wazayuni nusu milioni wa Israel wamekimbilia nje tangu kuanza vita vya Gaza
Jun 24, 2024 05:02Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Idadi ya Watu na Uhamiaji ya Israeli zimefichua kwamba zaidi ya Waisraeli nusu milioni wamekimbilia nje na hawajarejea tangu kuanza vita vya utawala huo kwenye Ukanda wa Gaza, mnamo Oktoba 7 mwaka jana.
-
Wakazi wa utawala wa Kizayuni waitisha mgomo mkubwa hadi Netanyahu aanguke
Jun 24, 2024 03:22Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limetangaza habari ya kuitishwa mgomo mkubwa zaidi wa maeneo yote ya utawala wa Kizayuni hadi serikali ya Benjamin Netanyahu itakapopigwa na chini.