-
Guterres: Nina wasiwasi mkubwa kuhusu ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa huko Gaza
Oct 24, 2023 23:48Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema: Hali katika Mashariki ya Kati (Asia Magharibi) inazidi kuwa mbaya na huenda vita vya Gaza vikaenea katika eneo hilo.
-
UNRWA: Hospitali za Gaza zinafungwa leo kutokana na kumalizika akiba ya mafuta
Oct 24, 2023 23:47Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limeonya kuwa utoaji huduma katika hospitali za Gaza utasimamishwa kutokana na kumalizika akiba ya mafuta katika eneo hilo.
-
Maelfu ya waliokimbia makazi yao na waliojeruhiwa huko Ghaza wanasubiri misaada ya dharura na matibabu
Oct 24, 2023 23:21Licha ya kuwa utawala wa Kizayuni, chini ya mashinikizo ya kimataifa, hatimaye umekubali kupelekwa misaada midogo ya kibinadamu huko Ghaza, na hayo ni baada ya kupitia ukaguzi unaochukua muda mrefu, lakini misaada hiyo haitoshi kabisa kukidhi mahitaji mengi ya watu wa Ghaza walio chini ya mashambulio makali na mzingiro wa kidhalimu wa utawala huo wa kibaguzi.
-
Ajuza Muisrael aliyekuwa mateka asimulia alivyokirimiwa na wapiganaji wa HAMAS+VIDEO
Oct 24, 2023 11:02Mwanamke mzee Muisrael aliyeachiliwa huru na wapiganaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema alikirimiwa na kutendewa wema katika muda wa wiki mbili alipokuwa ameshikiliwa mateka na kundi hilo la wanamapambano wa Palestina.
-
Amir wa Qatar: Dunia isiipe Israel leseni ya kuwaua Wapalestina
Oct 24, 2023 10:24Amir wa Qatar amesema anatiwa wasiwasi na hatua ya Israel ya kushadidisha jinai na mashambulizi katika Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na kuiasa jamii ya kimataifa isiupe leseni utawala huo wa Kizayuni ya kuwaua shahidi wananchi wa Palestina.
-
Walimwengu waendelea kuandama wakiwaunga mkono wananchi wa Palestina
Oct 24, 2023 03:52Waungaji mkono wa wananchi wa Palestina katika maeneo mbalimbali ulimwenguni wameendelea kujitokeza na kuandamana wakilaani jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza.
-
Mitetemo ya Kimbunga cha Al Aqsa ndani ya Israel
Oct 24, 2023 02:40Mgawanyiko na hitilafu zinazidi kuongezeka ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu tangu kuundwa serikali yenye misimamo mikali ya Netanyahu na kuenea hadi kwa raia wa kawaida; huku wafuasi wa makundi mawili ya kisekula na kidini wakikabiliana mara kadhaa hadi sasa na wakati mwingine wakijikita katika mapigano na kuibua ghasia.
-
Mpasuko waripotiwa katika baraza la mawaziri la utawala haramu wa Israel
Oct 23, 2023 22:56Gazeti la Israel la Yedioth Ahronoth limeripoti kuwa, kuna mgogoro wa kutoaminiana kati ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na uongozi wa jeshi lake, na kwamba uhusiano wake na Waziri wa Ulinzi katika serikali yake, Yoav Galant, unayumbayumba, jambo ambalo linazuia ushirikiano wa kikazi baina ya wawili hao.
-
Jihad Islami: Misimamo ya nchi za Kiarabu na Kiislamu ni dhaifu
Oct 23, 2023 22:49Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetangaza kuwa misimamo dhaifu ya nchi za Kiarabu na Kiislamu inazidisha mateso na masaibu kwa watu wa Ghaza.
-
Watu waliozingirwa Gaza wanasubiri msaada wa kimataifa
Oct 23, 2023 07:41Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema katika hotuba yake kwenye Kikao cha Amani cha Cairo: 'Tunakutana katikati ya eneo ambalo lina maumivu makali na limesimama hatua moja kutoka kwenye shimo refu. Eneo ambalo hauwezi kukosa kuhuzunika na kukereka na moyo kuuma na kusononeka kwa kuona picha za machungu na mateso ya watu wake.'