Walimwengu waendelea kuandama wakiwaunga mkono wananchi wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103874-walimwengu_waendelea_kuandama_wakiwaunga_mkono_wananchi_wa_palestina
Waungaji mkono wa wananchi wa Palestina katika maeneo mbalimbali ulimwenguni wameendelea kujitokeza na kuandamana wakilaani jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 24, 2023 03:52 UTC
  • Walimwengu waendelea kuandama wakiwaunga mkono wananchi wa Palestina

Waungaji mkono wa wananchi wa Palestina katika maeneo mbalimbali ulimwenguni wameendelea kujitokeza na kuandamana wakilaani jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza.

Jumatatu ya jana ilishuhudia maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali ya dunia ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina. Mjini Boston Marekani mamia ya Wamarekani waliandamana ambapo wakiwa wamebeba bendera za Palestina walipiga nara za kulaani mauaji ya Israel dhidi ya Wapalestina.

Maandamano kama hayo yamefanyika pia nchini Mauritania ambapo waandamanaji walikwenda na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Nouakchott ambapo sambamba na kutangaza mfungamano wao na Wapalestina walilaani himaya na uungaji mkono wa serikali ya Marekani kwa Israel inayofanya mauaji dhidi ya Wapalestina.

Aidha waandamanaji hao wamelaani vikali kimya chha madola ya Magharibi kwa mauaji na jinai za Israel dhidi ya wakazi wa Gaza na kutangaza kuwa, Marekani na madola ya Magharibi ni washirika wa jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika mataifa mbalimbali ya Ulaya kumefanyika maandamano ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina ukiwemo mji mkuu wa Italia Rome.

 

Aidha mji mkuu wa Ujerumani Berlin na ulishuhudia maandamano kama hayo ambapo polisi ya mji huo iliyatawanya maandamano hayo na kuwatia mbaroni waandamanaji kadhaa.

Bosnia Herzegovina na Denmark nazo zimeshuhudia maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina. Wafuasi wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Economic Freedom Fighters, wamefanya maandamano makubwa na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina. Kiongozi wa chama hicho, Julius Malema, kwa mara nyingine tena ametoa wito wa kufungwa ubalozi wa Israel nchini Afrika Kusini baada ya kusisitiza kuwa, utawala wa Israel "hauheshimu ubinadamu".