-
Kujikusanya tena wananchi wa Marekani kwa ajili ya kuunga mkono watu wa Gaza sambamba na Kongamano la Chama cha Kidemokrasia
Aug 20, 2024 10:41Baada ya mapumziko mafupi, wimbi la maandamano ya kuunga mkono watu wa Gaza na Palestina linaongezeka huko Marekani, na inaonekana kwamba mchakato huu utapata kasi na kasi zaidi wakati wanafunzi watakaporejea katika vyuo vikuu baada ya kumalizika likizo.
-
Chanzo cha Muqawama: Uingereza inashirikiana na Israel katika vita dhidi ya Gaza
Aug 20, 2024 08:31Chanzo cha habari katika Chumba cha Operesheni za Muqawama wa Palestina kimesema kuna ushahidi wa wazi kwamba Uingereza inakusanya habari za kijasusi huko Gaza kwa niaba ya utawala ghasibu wa Israel na kwamba kwa kufanya hivyo London inashiriki katika mauaji ya maelfu ya wanawake na watoto katika eneo hilo la Palestina.
-
Juhudi za wajumbe wa Kiislamu katika Kongamano la Kitaifa la Democratic kwa ajili ya kuiwekea vikwazo Israel
Aug 20, 2024 02:26Makumi ya wajumbe na makundi ya Kiislamu yanayokerwa na uungaji mkono wa Marekani kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza, wanapanga kufanya mabadiliko katika mpango wa uchaguzi wa Chama cha Democratic na kutilia mkazo suala la kuwekwa vikwazo vya silaha dhidi ya Israel.
-
Maandamano ya kuiunga mkono Palestina yafanyika Chicago
Aug 19, 2024 23:14Katika kukaribia kufanyika kongamano la kitaifa la chama cha Democrat nchini Marekani idadi kubwa ya wananchi wanaopinga sera za kupenda vita za serikali ya Washington na uungaji mkono wake kwa utawala wa Kizayuni katika vita vya Gaza wameandamana katika mji wa Chicago kwa lengo la kuiunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni.
-
OCHA: Wafanyakazi 280 wa huduma za kibinadamu waliuawa mwaka 2023
Aug 19, 2024 22:44Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imetangaza kuwa, wafanyakazi 280 wa utoaji huduma za kibinadamu waliuawa kwenye mataifa 33 katika mwaka uliiopiita wa 2023.
-
The Independent: 92% ya Waislamu wa Uingereza hawana amani
Aug 18, 2024 23:27Uchunguzi wa maoni uliofanywa na kuchapishwa na gazeti la The Independent la Uingereza unaonyesha kuwa, asilimia 92 ya Waislamu wa nchi hiyo hawahisi kuwa na amani.
-
Maandamano ya kulaani jinai za Israel yafanyika tena nchini Ujerumani
Aug 18, 2024 23:19Maelfu ya wananchi wa mji mkuu wa Ujerumani Berlin wameandamana tena wakilaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wapalestina hususan wa Ukanda wa Gaza.
-
Onyo la Guterres kuhusu mporomoko wa ubinadamu huko Gaza
Aug 18, 2024 22:48Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameonya kwamba eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina liko katika "mporomoko huru wa ubinadamu". Guterres ameyasema hayo akizungumzia hali mbaya na mgogoro mkubwa unaowasumbua na kuwatesa wakazi wa eneo hilo.
-
Kamala Harris akiri kutoridhishwa wananchi wa Marekani na hali ya uchumi
Aug 18, 2024 03:40Kamala Harris mgombea wa uchaguzi wa rais kwa tiketi ya chama cha Democrat nchini Marekani amekiri kuwa wananchi wa nchi hiyo hawaridhishwi na mfumuko wa bei za bidhaa na gharama kubwa za maisha na ameahidi kudhibiti mfumuko huo.
-
Cuba yataka kuwajibishwa Israel mkabala wa jinai zake katika Ukanda wa Gaza
Aug 18, 2024 03:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba ametaka kuhitimishwa kinga kwa utawala wa Kizayuni na akisema Israel inapasa kuwajibishwa kwa jinai ilizotenda katika Ukanda wa Gaza.