-
Russia: Hakuna mazungumzo ya kusitisha mapigano mkesha wa Mwaka Mpya
Dec 03, 2025 03:06Msemaji wa Ikulu ya Russia, Kremlin, amesema kuwa, hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kuhusu kusimamishwa vita wakati wa mkesha wa X-Mass na mwaka mpya huko Ukraine.
-
Putin: Tuko tayari kupigana na Ulaya kama itataka vita
Dec 02, 2025 23:47Rais wa Russia, Vladimir Putin, ameishambulia vikali Ulaya katika matamshi yake ya jana Jumanne, akitangaza utayarifu wa nchi yake kupigana vita dhidi Ulaya, anayoituhumu kuwa inafanya jitihada za kuharibu makubaliano ya kusimamisha mapigano nchini Ukraine na kuishinda Russia kistratijia.
-
Maduro aapa Venezuela haitakubali "amani ya utumwa" ya Marekani
Dec 02, 2025 23:20Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, amesema Caracas haitainama mbele ya shinikizo la kijeshi na kisiasa kutoka Washington, akisisitiza taifa hilo linapinga aina yoyote ya amani ambayo ni sawa na "utumwa" kwa Marekani.
-
WHO yaafiki matumizi ya dawa za kupunguza uzito, utipwatupwa ni ugonjwa sugu
Dec 02, 2025 23:17Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limetoa mwongozo wake wa kwanza kuhusu matumizi ya kundi jipya la dawa za kupunguza uzito, hatua inayowakilisha mabadiliko makubwa katika sera za afya duniani wakati viwango vya unene wa kupitiliza au utipwatupwa vikizidi kuongezeka.
-
Kwa nini Marekani inafanya njama za kuidhibiti Venezuela?
Dec 02, 2025 03:45Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amesisitiza kuwa, nchi yake itaendelea kulinda rasilimali zake kwa nguvu zote mbele ya tamaa ya kuchupa mipaka ya Marekani.
-
Papa Leo: Kuundwa taifa la Palestina ndio suluhisho pekee la amani
Dec 02, 2025 03:25Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, ambaye alikuwa safarini huko Beirut nchini Lebanon, amesema kwamba kuundwa taifa la Palestina ndio chaguo pekee linaloweza kuhakikisha haki kwa Wapalestina na Waisraeli.
-
ICC: Vikwazo vya Marekani vimewaathiri majaji, hatutasalimu amri kwa shinikizo lolote
Dec 02, 2025 02:54Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), Jaji Tomoko Akane, amesema kwamba vikwazo vya Marekani vilivyowekwa dhidi ya maafisa wakuu na majaji wa mahakama hiyo vimeathiri moja kwa moja maisha binafsi ya majaji na maafisa walengwa.
-
Afisa wa jeshi la Uingereza: Tuliua makumi ya Waafghani, maafisa walificha uhalifu huo
Dec 01, 2025 23:54Afisa wa zamani wa jeshi la Uingereza amefichua mauaji yaliyofanywa na askari wa kikosi maalumu cha Uingereza nchini Afghanistan na jinsi makamanda wa kikosi hicho walivyonyamazia kimya na kuficha uhalifu huu.
-
Kwa nini umma unapaza sauti zaidi katika mitaa ya Paris kupinga migongano ya sera za Ulaya?
Dec 01, 2025 23:10Makumi ya maelfu ya watu huko Paris, mji mkuu wa Ufaransa, wametoa kauli mbiu "Muqawama; kutoka Paris hadi Palestina; wakiunga mkono Wapalestina.
-
Watu 1,000 wafariki dunia katika mafuriko Indonesia, Sri Lanka, Thailand, Malaysia
Dec 01, 2025 06:56Mafuriko mabaya yaliyozikumba nchi za Indonesia, Sri Lanka, Thailand na Malaysia yamepelekea zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha katika kipindi cha chini ya wiki moja. Kwa uchache watu 502 wameripotiwa kufariki dunia nchini Indonesia, 335 nchini Sri Lanka, 176 nchini Thailand na watatu nchini Malaysia.