Nafasi muhimu ya Afrika katika soko la nishati duniani
Gazeti la Economist limetabiri kuwa Afrika itakuwa na nafasi muhimu katika soko la nishati duniani katika siku zijazo kutokana na rasilimali zake nyingi za gesi asilia, mwanga wa jua na upepo.
Gazeti la Economist limeashiria katika ripoti yake kuhusu wasiwasi wa usalama wa nishati kutokana na kusitishwa kwa uuzaji wa gesi ya Russia kwa nchi za Ulaya; ikiwa ni natija ya vita vya Ukraine na kuongezeka bei ya nishati duniani na kuandika kuwa: Matukio haya yanaripotiwa huku mabadiliko ya tabianchi yakisababisha taathira kubwa katika matumizi ya nishati ya mafuta kama vile mafuta na gesi.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Afrika inaweza kuwa jibu kwa matatizo ya dharura ya gesi yanayozikabili nchi za Ulaya na tatizo la muda mrefu la gesi ya kaboni barani humo.
Afrika ina asilimia 13 ya akiba ya gesi duniani, ambayo ni kidogo kulinganisha na ile ya Asia ya Maghaŕibi, na ina asilimia saba ya akiba ya mafuta huku pia ikiwa na uwezo mzuri katika suala la nishati ya kijani.