Oct 21, 2023 03:01 UTC
  • Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania yatoa tamko juu ya mgogoro wa Palestina

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanaznia Sheikh Alhaad Mussa Salim ametoa tamko kwa Umoja wa Mataifa na jumuiya mbalimbali za kimataifa ili kuingia kati na kusitisha vita kati ya Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Alhaad Mussa amesema kuwa kadhia ya vita kati ya Israel na Palestina ni ya muda mrefu na akasema, yanayotokea sasa ni uvunjaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa.

Sheikh Alhaad Mussa 

Amesema wamehuzunushwa sana kama wapenda amani duniani kuona nyumba za ibada, hospitali, makazi ya watu yakipigwa mabomu na kuharibiwa huduma za msingi za kibinadamu kama umeme na maji.

Amesema kwa hiyo wanaziomba mamlaka husika hasa Umoja wa Mataifa na Jumuiya za Kimataifa zihakikishe usitishwaji vita unatekelezwa mara moja sambamba na kuhakikisha huduma za kibinadamu kama umeme, maji na matibabu zinarejeshwa mara moja.

 

Tags