Zimbabwe imeshindwa kulilipa jeshi kwa mwezi wa pili mfululizo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11329-zimbabwe_imeshindwa_kulilipa_jeshi_kwa_mwezi_wa_pili_mfululizo
Zimbabwe imeshindwa kulipa mishahara ya jeshi la nchi hiyo kwa wakati kwa mwezi wa pili mfululizo sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 16, 2016 00:02 UTC
  • Zimbabwe imeshindwa kulilipa jeshi kwa mwezi wa pili mfululizo

Zimbabwe imeshindwa kulipa mishahara ya jeshi la nchi hiyo kwa wakati kwa mwezi wa pili mfululizo sasa.

Kwa kawaida jeshi la Zimbabwe hulipwa mishahara tarehe 14 ya kila mwezi hata hivyo wanajeshi na maafisa wa Jeshi la Anga la nchi hiyo wamesema kuwa bado hawajapokea mishahara na wala hawajapewa taarifa lini watalipwa mishahara yao.

Ucheleweshaji huo wa mishahara ya jeshi la Zimbabwe unatazamia kuchochea hali ya mivutano nchini humo ambayo tayari imekumbwa na ukame, kushuka kwa bei za madini na uhaba mkubwa wa fedha; masuala ambayo yote yamesababisha maandamano mwezi huu nchini humo dhidi ya Rais Robert Mugabe.

Waziri wa Fedha wa Zimbabwe Patrick Chinamasa ambaye anashiriki katika mkutano wa Umoja wa Afrika huko Rwanda pamoja na Rais Mugabe hajatoa maelezo yoyote kuhusu lini wanajeshi watalipwa mishahara yao.