Aug 10, 2024 12:54 UTC
  • Watu 30 wauawa katika shambulio la wanamgambo nchini Nigeria

Kwa akali watu 30 wameuawa katika jimbo la Benue nchini Nigeria baada ya kundi la wanamgambo kufanya mashambulio dhidi ya kijiji cha Ayati.

Mbali na kuua takriban watu 30, majambazi na waasi walishambulia kijiji kimoja katika jimbo la Benue nchini Nigeria na kupora mali za wanakijiji hao.

Ripoti zinaeleza kuwa, kuna uwezekano wa kuongezeka idadi ya wahanga wa shambulio hilo kwani juhudi za kusaka miili ya wahanga wa shambulio hilo zinaendelea. Viongozi wa Nigeria wamelaani vikali shambulio hilo na kutoa wito wa kufanyika uchunguzi wa tukio hiilo.

Tangu mwaka 2009, Boko Haram imekuwa ikifanya na mashambulizi makubwa ya kigaidi nchini Nigeria na kusababisha vifo vya zaidi ya 20,000.

Genge hilo limepanua wigo wa mashambulizi yake hadi nchi jirani za Cameroon, Chad na Niger tangu mwaka 2015, na kusababisha kuuawa kwa uchache watu 2,000 wengine katika eneo la Bonde la Ziwa Chad.

Mamia kwa maelfu ya Wanigeria huwa wanakimbia makazi yao kila mwaka kutokana na mashambulizi ya kigaidi na migogoro inayoendelea kwenye maeneo yao.

Tags