Mshukiwa wa mauaji ya makumi ya wanawake Kenya atoroka gerezani
Raia wa Kenya aliyekiri kuhusika na mauaji ya wanawake 42 ambao baadhi yao miili yao ilipatikana imetupwa katika eneo la kutupa taka jijini Nairobi, ametoroka gerezani.
Taarifa ya Polisi ya Kenya imesema, Collins Jumaisi, 33, ametoroka gerezani pamoja na wafungwa wengine kadhaa.
Jumaisi alikamatwa na polisi mwezi uliopita baada ya miili ya wanawake waliokatakatwa vipande kupatikana ikiwa imetupwa kwenye eneo la taka katika mtaa wa Embakasi, nje kidogo na jiji la Nairobi.
Msemaji wa Polisi ya Kenya amesema, wafungwa 13 walitoroka gerezani usiku wa kuamkia leo Jumanne, akiwemo mshukiwa mkuu wa mauaji ya wanawake hao.
Miongoni mwa wafungwa waliotoroka ni pamoja na raia 13 wa Eriteria.
Collins Jumaisi alifikishwa mahakamani Ijumaa ya wiki iliopita ambapo hakimu aliagiza azuiliwe kwa muda wa miezi 30 zaidi kutoa nafasi ya uchunguzi kamili.
Mwezi uliopota wa Julai Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) ilitangaza kwamba mshukiwa huyo mkuu wa mauaji ya eneo la Kware, mtaa wa Mukuru Kwa Njenga, viungani mwa Nairobi amekiri kuua zaidi ya wanawake 40.