UN yazikosoa nchi za Ulaya kwa kuondoa majeshi yao Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11656-un_yazikosoa_nchi_za_ulaya_kwa_kuondoa_majeshi_yao_sudan_kusini
Umoja wa Mataifa umezikosoa nchi tatu za Ulaya kwa kuondoa askari wao katika nchi iliyotumbukia tena katika mapigano ya ndani ya Sudan Kusini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 21, 2016 01:12 UTC
  • UN yazikosoa nchi za Ulaya kwa kuondoa majeshi yao Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umezikosoa nchi tatu za Ulaya kwa kuondoa askari wao katika nchi iliyotumbukia tena katika mapigano ya ndani ya Sudan Kusini.

Ripoti iliyotolewa jana na Umoja wa Mataifa imezikosoa nchi za Uingereza, Ujerumani na Sweden kwa kuchukua uamuzi huo na kutangaza kuwa, nchi hizo zilizokuwa na askari katika kikosi cha kulinda amani Sudan Kusini zimechukua uamuzi wa kuwarejesha nyumbani askari wao bila ya kushauriana na Umoja wa Mataifa. 

Farhan Haq

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema baada ya kushadidi mapigano ya ndani nchini Sudan Kusini, askari 140 wa kulinda amani wa umoja huo wameondoka katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.

Sudan Kusini imetumbukia tena katika mapigano makali kuanzia mwezi uliopita wa Juni licha ya pande mbili hasimu kutia saini makubalino ya kusitisha vita na kugawana madaraka. Mapigano hayo yanahusisha waasi wanaoongozwa na Makamu wa Rais, Riek Machar na askari watiifu kwa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini. 

Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa hadi sasa katika mapigano hayo.