Mahakama Ghana yabatilisha uamuzi wa kusitisha shughuli za Bunge
(last modified Fri, 01 Nov 2024 02:27:24 GMT )
Nov 01, 2024 02:27 UTC
  • Mahakama Ghana yabatilisha uamuzi wa kusitisha shughuli za Bunge

Mahakama ya juu nchini Ghana imebatilisha uamuzi ambao ulikuwa umepelekea kusitishwa shughuli za bunge miezi michache kabla ya uchaguzi.

Hatua hiyo ilisitisha kikamilifu shughuli zote za kisheria miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, ambao unatarajiwa kuwa kinyang'anyiro kikali wakati ambapo nchi hiyo inajaribu kujifufua kiuchumi kufuatia mzozo mkubwa wa kifedha.

Jaji Mkuu Gertrude Torkornoo, amesema kuwa, kwa kuzingatia madhara yasiyoweza kurekebishwa ambayo yanaweza kuyakumba maeneo ya bunge yalio na maelfu ya raia wa nchi hiyo, ilikuwa muhimu kwa mahakama hiyo kushughulikia mzozo huo mara moja.

Mgogoro huo ulichochewa na msuguano kati ya chama tawala cha Rais Nana Akufo-Addo cha New Patriotic Party (NPP) na chama cha upinzani cha National Democratic Congress (NDC) kilichopata ushindi mdogo baada ya wabunge wanne kujitoa.

Uamuzi mwa Mahakama ya Juu sasa unatarajiwa kuhitimisha kile kilichokuuwa kimepelekea kuibuka mvutano mkuubwa baina ya chama tawala na mrengo wa upinzani nchini Ghana.