Waziri Tuggar: Nigeria inaunga mkono juhudi za ukombozi wa Palestina
(last modified Tue, 19 Nov 2024 02:41:31 GMT )
Nov 19, 2024 02:41 UTC
  • Waziri Tuggar: Nigeria inaunga mkono juhudi za ukombozi wa Palestina

Yusuf Maitama Tuggar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Nigeria amesema kuwa nchi yake ingali inaunga mkono juhudi za kisiasa na kiuchumi za ukombozi wa Palestina.

Yusuf Maitama Tuggar amesisitiza kuwa, Nigeria itaendelea kuunga mkono Palestina dhidi ya miongo kadhaa ya uvamizi na ukaliaji mabavu Israel, sawa na uungaji mkono wake wa kihistoria kwa harakati za ukombozi za Afrika Kusini, Angola, Msumbiji, Zimbabwe na Namibia kutoka kwa ukoloni wa Magharibi.

Aidha ameeleza kuwa, Rais Tinubu wa nchi hiyo amekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu mateso ya binadamu huko Gaza, hasa miongoni mwa watoto na wanawake.

Akizungumzia unafiki unaofanywa na vyombo vya habari vya Magharibi, Yusuf Maitama Tuggar alisisitiza ujumbe wa Rais Bola Ahmad Tinubu katika Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) na Araba League nchini Saudi Arabia mnamo Novemba 11 ambapo alisitiza kuwa mzozo huo haukuanza Oktoba 7, 2023.

Nigeria ni miongoni mwa mataifa ambayo yamekuuwa yakitoa himaya na uungaji mkono kwa Palestina na kumekuwa kukishuhudiwa maandamano ya mara kwa mara ya kulaani jinai za Israel na kutangaza kuwa pamoja na Wapalestina.