Wanamgambo wa CODECO washambulia na kuuwa zaidi ya watu 35
Wanamgambo wenye silaha wamewaua zaidi ya raia 35 na kuwajeruhi wengine kadhaa, katika shambulio lililotokea usiku wa Jumatatu katika vijiji vya baadhi vya jimbo la Ituri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kiongozi wa kundi la Djaiba katika vijiji vya Djugu Jean Vianney amesema, wanamgambo wa CODECO walitekeleza shambulizi hilo ambalo lilianza majira ya saa mbili usiku, wakiwauwa wakaazi kwa kuwapiga risasi na kuziteteteza nyumba zao kwa moto.
Vianney amesema "tumewahesabu zaidi ya watu 35 waliokufa majira ya asubuhi hii leo, na juhudu za kutafuta wahanga zikiendellea." Alisema.
Aidha aliongeza kwamba wapo watu waliojeruhiwa vibaya, wengi wamepoteza maisha kutokana na kuungua na moto ndani ya nyumba zao.
Ama katika upande mwingine kiongozi wa asasi za kiraia katika eneo hilo Jules Tsuba amesema miili 49 ilipatikana hadi kufikia asubuhi ya leo Jumanne, katika wakati ambapo bado juhudi za kutafuta waathirika zaidi zikiendelea kuchukuliwa.
Umoja wa Mataifa umewahi kuwashutumu kwa mashambulizi dhidi ya jamii nyingine, ikiwemo wafugaji wa Hema, mashambulizi yanayoweza kuhesabiwa kama uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Wengi wa waathirika katika mkasa huo kwa mujibu wa kiongozi wa Djaiba ni pamoja na watu wa jamii ya Hema, huku akiongeza kwamba mashambuliozi hayo yamefanyika wakati ambapo wanajeshi wa Kongo pamoja na walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakiwa umbali wa takriban kilometa tatu, hivyo hawakupata masaada wa haraka.
Wakati hayo yakiendelea duru za kisiasa na kidiplomasia zinaripoti kwamba Afrika kusini imetuma zaidi wanajeshi pamoja na zana za kijeshi kuelekea mashariki mwa Kongo katika siku za hivi karibuni, ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya wanajeshi wake 14 kuuwawa katika mapigano na waasi wa M23.