Wamorocco waandamana dhidi ya waziri wa utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i123076-wamorocco_waandamana_dhidi_ya_waziri_wa_utawala_wa_kizayuni
Wananchi wenye hasira wa Morocco wameandamana kupinga uwepo wa Waziri wa Usafirishaji wa utawala wa Kizayuni katika kongamano la kimataifa nchini Morocco.
(last modified 2025-02-22T23:12:31+00:00 )
Feb 22, 2025 23:12 UTC
  • Wamorocco waandamana dhidi ya waziri wa utawala wa Kizayuni

Wananchi wenye hasira wa Morocco wameandamana kupinga uwepo wa Waziri wa Usafirishaji wa utawala wa Kizayuni katika kongamano la kimataifa nchini Morocco.

Mkutano wa Kimataifa wa Usalama Barabarani ulifanyika wiki iliyopita katika mji wa Marrakesh Kaskazini mwa Morocco, na Miri Regev, Waziri wa Usafirishaji wa utawala wa Kizayuni alishiriki katika mkutano huo.

Wananchi wa miji mbalimbali ya Morocco walijitokeza katika mitaa na barabara na kuandama kulalamikia safari ya waziri huyo wa utawala wa Kizayuni katika nchi yao.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walitangaza upinzani wao pia dhidi ya mpango wa Trump wa kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina w na walisikika wakipiga nara: "Katika zama za uhuru, Gaza inapinga kuhanmishwa watu kwa nguvu.

Mnamo Desemba 2020, Morocco na Israel zilitangaza kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baada ya kusimamishwa mwaka 2000 kufuatia kuzuka kwa Intifadha ya pili ya Palestina.

Morocco ilikuwa nchi ya nne ya Kiarabu kukubali kurejesha uhusiano na Israel mwaka 2020 baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan. Wananchi wa Morocco wamejiunga na wenzao katika nchi za Kiarabu kupinga vikali uamuzi wa serikali zao kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel na wametaka mapatano ya kuanzisha uhusiano huo yafutwe.