Mafuriko Msumbiji: Maelfu wapoteza makazi huku shule zikifungwa
(last modified Sun, 23 Feb 2025 07:46:48 GMT )
Feb 23, 2025 07:46 UTC
  • Mafuriko Msumbiji: Maelfu wapoteza makazi huku shule zikifungwa

Mafuriko makubwa yaliyoiathiri Botswana yamesababisha vifo vya watu saba wakiwemo watoto watatu na kuharibu nyumba za maelfu ya watu baada ya siku kadhaa za mvua kubwa kunyesha kote nchinu humo. Haya yamebainishwa jana na Rais Duma Boko wa nchi hiyo.

Amesema mamlaka husika za Botswana zimefunga kwa muda shule kufuatia mvua kubwa zilizosababisha mafuriko ambazo zimenyesha katika maeneo mbalimbali nchini humo kwa zaidi ya wiki moja. 

"Tutaendelea kufanya kazi ili kuzuia maafa zaidi," amesema Rais Boko wa Botswana akilihutubia taifa  baada ya watu 1,700 kuhamishwa katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko. 

Katika mji mkuu, Gaborone, ambako bwawa la eneo hilo limezidiwa na wingi wa maji ya mafuriko; magari na mali za zimesombwa na maji, huku wafanyakazi wa huduma za ukoaji na dharura wakijiandaa kwa mvua zaidi siku zijazo.

Maafisa wa Idara ya Kukabiliana na Maafa ya Botswana wamesema kuwa uhaba wa mifereji ya kupitishia maji katika maeneo ya mijini huwenda imechangia maji kuongezeka katika baadhi ya maeneo ya mabondeni yaliyoathirika zaidi.

Rais Duma Boko wa Botswana amesema kuwa mamlaka husika za nchi hiyo zinapasa kutazama upya iwapo miundombinu katika ngazi ya kitaifa inaweza kukabiliana na ukame pamoja na mafuriko au la.