Jumanne, 21 Januari, 2025
Leo ni Jymanne tarehe 20 Rajab 1446 Hijria mwafaka na tarehe 21 Januari 2025.
Miaka 1433 iliyopita katika siku kama hii ya leo, vilitokea vita vya Yarmuk kati ya jeshi la Kiislamu na jeshi la utawala wa kifalme wa Roma ya Mashariki katika bonde lililojulikana kwa jina hilo huko Palestina.
Ushindi wa Waislamu huko Sham, yaani Syria ya sasa ulimpelekea mfalme wa Roma kuandaa jeshi kubwa kwa ajili ya kupigana na Waislamu. Lakini, Waislamu waliweza kutoa pigo kwa wanajeshi wa mfalme wa Roma licha ya kuwa na idadi ndogo ya wapiganaji na suhula chache za kivita.
Kufuatia ushindi huo Waislamu walisonga mbele na kufika eneo la Mashariki la Ufalme wa Roma na mwaka mmoja baada ya hapo jeshi la Kiislamu lilifanikiwa kuchukua udhibiti wa mji wa Baitul Muqaddas pasina umwagaji damu. ***
Katika siku kama ya leo miaka 289 iliyopita tufani kubwa ililikumba eneo la Ghuba ya Bengali mashariki mwa India na kuua watu laki tatu.
Tufani hiyo ilitambuliwa kuwa kimbunga kilichosababisha maafa makubwa zaidi katika eneo hilo.
Ghuba ya Bengali iko kaskazini mwa Bahari ya Hindi na kusini mwa Asia na ni miongoni mwa maeneo ambayo hukumbwa na mafuriko na vimbunga vya mara kwa mara vinavyosababisha maafa makubwa ya nafsi na mali.

Siku kama ya leo miaka 232 iliyopita Mfalme Louis XIV wa Ufaransa alinyongwa.
Alichukua hatamu za uongozi mwaka 1774 na kuathiriwa mno na mkewe Marie-Antoinette. Mwaka 1789 wananchi wa Ufaransa walianzisha mapambano dhidi ya Mfalme Louis XIV kutokana na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii na miaka mitatu baadaye serikali ya kifalme ilifutwa rasmi nchini Ufaransa.
Hata hivyo kutokana na kuwa mfalme Louis alikuwa ameomba msaada wa nchi za kigeni kwa siri alituhumiwa kuwa amefanya uhaini na kuhukumiwa kifo. Watu kadhaa wa familia ya Mfalme Louis XIV akiwemo mkewe Marie-Antoinette pia walinyongwa.

Miaka 46 iliyopita katika siku inayosadifiana na hii ya leo, ikiwa ni katika mwendelezo wa wananchi Waislamu wa Iran kupinga utawala wa Shah na kukabiliana na wanajeshi wa utawala huo, idadi kubwa ya raia waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Wananchi wa Iran ya Kiislamu wambao walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa kurejea nchini Imam Khomeini (M.A) walitayarisha mazingira hitajika kwa ajili ya mapokezi makubwa zaidi ya kihisitoria kwa kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Kwa mnasaba huo, wafanyakazi mbalimbali wakiwemo maulamaa na wawakilishi wa matabaka mbalimbali ya wakazi wa mji wa Tehran walikusanyika pamoja ili kuandaa hafla kubwa ya kumpokea Imam.
Watu wengi kutoka katika miji na vijiji vya Iran ya Kiislamu walimiminika kwa wingi mjini Tehran kwa lengo la kushiriki katika sherehe za kumkaribisha Imam Khomeini (M.A).
Katika upande mwingine, baada ya maandamano makubwa ya wananchi, wanajeshi elfu nne wa jeshi la anga pia waligoma kula wakitaka kuondoka Iran washauri wa kijeshi wa Marekani katika kuwaunga mkono wananchi wanapambano wa Iran.
