Harakati ya Kiislamu Nigeria yawaenzi na kuwaomboleza viongozi wa muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i123136-harakati_ya_kiislamu_nigeria_yawaenzi_na_kuwaomboleza_viongozi_wa_muqawama
Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria katika Jimbo la Kano imewaenzi na kuwaomboleza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyed Hassan Nasrullah na Mkuu wa zamani wa Baraza la Utendaji la harakati hiyo, Sayyed Hashem Safieddine, waliouawa shahidi katika shambulio la anga la Israel huko Beirut.
(last modified 2025-02-24T03:43:37+00:00 )
Feb 24, 2025 03:43 UTC
  • Harakati ya Kiislamu Nigeria yawaenzi na kuwaomboleza viongozi wa muqawama

Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria katika Jimbo la Kano imewaenzi na kuwaomboleza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyed Hassan Nasrullah na Mkuu wa zamani wa Baraza la Utendaji la harakati hiyo, Sayyed Hashem Safieddine, waliouawa shahidi katika shambulio la anga la Israel huko Beirut.

Sheikh Sunusi Abdulqadir, mwakilishi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky katika Jimbo la Kano akitoa hutuba katika hadhara hiyo alisema, "Leo tuko hapa sio kuelezea huzuni au malalamiko, bali kuuambia ulimwengu kwamba hakika tutatimiza ahadi zetu za kuendeleza mapambano katika njia ya muqawama, njia ya Imamu Husein na njia ya Sayyed Hassan Nasrullah."

Ameongeza kuwa, kumbukumbu na urithi wa Sayyed Nasrullah utaendelea kuishi hadi mwisho wa Waisraeli na kila aina ya dhulma duniani.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilifanya kumbukumbu kama hiyo ya kuwaenzi mashahidi hao wa muqawama katika miji mingine ya Nigeria kama Abuja, Katsina, Yobe, Kaduna, Sokoto, Bauchi, Jos na Gombe.

Kwa uoande wake, Kiongozi wa Waislamu wa madhebeu ya Shia nchini Nigeria amesisitiza kuwa, kushiriki mamilioni ya watu katika mazishi ya Mashahidi wa Muqawama ni sawa na "kuzaliwa upya Muqawama wa Lebanon".

Sheikh Ibrahim Zakzaky, ambaye yuko Beirut alikokwenda kuhudhuria mazishi ya Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiyyuddin, amesema katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa hapo jana na mwandishi wa Shirika la Habari la Mehr aliyetumwa huko Lebanon kwamba kuhudhuria mamilioni ya watu katika mazishi ya makamanda wa Muqawama kunadhihirisha kuwa Muqawama umezaliwa upya nchini Lebanon.