Imebainika: Ugonjwa "usiojulikana" ulioua makumi ya watu Congo DR ni malaria
Imebainika kuwa vifo vya makumi ya watu na mamia ya visa vilivyozua hofu katika jimbo la Equateur nchini Congo DR vimehusishwa na ugonjwa wa malaria. Awali iliripotiwa kuwa vifo hivyo viimesababishwa na ugonjwa usiojulikana.
Mamia ya watu wamegunduliwa kuwa na ugonjwa wa malaria kaskazini-magharibi mwa Congo huku mamlaka ya afya ikichunguza sababu za kuongezeka kwa kesi ambazo zimezidi 1,000 na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 60.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza kuwa japokuwa ugonjwa wa malaŕia, unaosambazwa na mbu, ni jambo la kawaida katika jimbo la Equateur nchini Kongo, lakini kuna uwezekano wa kuwepo sababu nyingine za vifo hivyo.
“Uchunguzi wa kina wa magonjwa, pamoja na uchunguzi wa ziada wa kimaabara, bado unahitajika,” imesema ofisi WHO barani Afrika.
Karibu kesi 1,100 zimerekodiwa tangu milipuko ya awali kutambuliwa katika vijiji viwili vya jimbo la Equateur mwishoni mwa Januari.