Vita vyaangamiza moja ya turathi wa kale zaidi nchini Sudan
Soko la Omdurman, ni moja ya masoko makongwe na la kihistoria nchini Sudan, ambalo lilianza takriban karne mbili zilizopita na linajulikana kama alama ya ustaarabu na mshikamano wa makabila tofauti nchini Sudan lakini sasa limeharibiwa vibaya.
Soko hili dogo, ambalo linachukuliwa kuwa "mfano wa mji mkuu wa kitaifa wa Sudan," lilikuwa ni mahali ambapo Wasudan, Wahindi na Wakristo walikuwa wanaishi na kufanya kazi pamoja, kwa utulivu, kuvumiliana na kwa amani.
Huko nyuma soko hilo la kale lilikuwa ni ishara ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya makabila mbalimbali; lakini sasa, baada ya kuzuka mapigano kati ya Jeshi la Sudan SAF na Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF, hali imebadilika kabisa. Uharibifu wa kitaasisi wa soko hili unaodaiwa kufanywa na RSF umelifanya soko hilo kuwa magofu na kutumbukia kwenye hali mbaya na ya ukiwa tofauti kabisa na ilikuwa kabla ya vita.
Maduka mengi yameharibiwa kabisa na vifaa na bidhaa zote zimeporwa. Pia, mabasi yaliyokuwa yakijaza eneo hilo la mraba hayapo tena ikiwa ni ishara tosha kwamba harakati za maisha hazipo tena kwenye soko hilo.
Lakini hivi sasa vita vya kutumia mizinga vimesita huko Omdurman. Hilo linaashiria kuweko mwanga wa matumaini kwamba maisha yatarejea katika hali ya kawaida kwenye mji huo na nchini Sudan kiujumla. Shughuli za ujenzi zimeanza hatua kwa hatua na maisha katika mji huo yameanza kurejea kwenye hali yake ya kawaida, licha ya uharibifu mkubwa unaoshukudiwa kwenye kila kochochor nakona za mji huo muhimu nchini Sudan.