Afrika Kusini yasisitiza tena msimamo wake kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel, Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i129372
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kwa mara nyingine tena amesisitiza kuhusu msimamo wa nchi hiyo katika faili la kesi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Gaza na kusema: Afrika Kusini inaitaka Israel isimamishe vita haraka iwezekanavyo huko Gaza, iruhusu misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo, iache kulikalia kwa mabavu eneo hilo na iache kuiaadhibu jamii ya Wapalestina.
(last modified 2025-08-10T09:22:10+00:00 )
Aug 10, 2025 09:22 UTC
  • Afrika Kusini yasisitiza tena msimamo wake kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel, Gaza

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kwa mara nyingine tena amesisitiza kuhusu msimamo wa nchi hiyo katika faili la kesi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Gaza na kusema: Afrika Kusini inaitaka Israel isimamishe vita haraka iwezekanavyo huko Gaza, iruhusu misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo, iache kulikalia kwa mabavu eneo hilo na iache kuiaadhibu jamii ya Wapalestina.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema katika Bunge la nchi hiyo kwmba: Kesi iliyowasilishwa na nchi hiyo dhidi ya utawala wa Israel  katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu mauaji ya kimbari ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza bado inaendelea. 

Rais Ramaphosa ameeleza kuwa serikali ya Afrika Kusini itaendelea kufuatilia kesi hiyo ya kisheria na kubainisha: "Hatujapokea ombi lolote rasmi kutoka kwa Marekani la kutazama upya kesi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel." 

Mwezi Disemba 2023, Afrika Kusini iliwasilisha kesi dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ikiituhumu Israel kuwa imekiuka Mkataba unaozuia mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.