Uganda inapanga kuwaondoa wanajeshi wake katika kikosi cha kulinda amani Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i135964-uganda_inapanga_kuwaondoa_wanajeshi_wake_katika_kikosi_cha_kulinda_amani_somalia
Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema nchi yake inapanga kuondoa wanajeshi wake huko Somalia baada ya kuwepo huko kwa kipindi cha miaka 19.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 27, 2026 10:06 UTC
  • Jenerali Muhoozi Kainerugaba
    Jenerali Muhoozi Kainerugaba

Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema nchi yake inapanga kuondoa wanajeshi wake huko Somalia baada ya kuwepo huko kwa kipindi cha miaka 19.

 Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema katika taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti yake ya jukwaa la X kwamba kazi ya Uganda nchini Somalia imefikia kikomo, na kwamba maandalizi ya kuondoka kikamilifu wanajeshi yataanza hivi karibuni.

Tangazo hili linakuja huku kukiwa na changamoto zinazoongezeka za kifedha zinazokabili Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM), ambao unachangia kudumisha amani na usalama wa Somalia na kupambana na harakati za kundi la al-Shabaab.

Bado hakujatangazwa ratiba rasmi ya kuondoka wanajeshi wa Uganda huko Somalia, na haijulikani jinsi hatua hiyo itakavyoathiri shughuli za Ujumbe wa Umoja wa Afrika (AMISOM) au hali ya usalama kwa ujumla nchini Somalia.

Uganda ilichangia kikosi kikubwa zaidi katika operesheni ya AMISOM, na ina wanajeshi wanaokadiriwa kufikia 6,000 nchini Somalia.