Wanajeshi kadhaa wauawa kaskazini mashariki mwa Libya
Aug 21, 2016 23:28 UTC
Vyombo vya habari vya nchi za Kiarabu vimeripoti habari ya kuuawa wanajeshi kadhaa wa Jenerali Khalifa Haftar katika mripuko wa bomu uliotokea kaskazini mashariki mwa Libya.
Duru hizo zimeripoti kuwa wanajeshi sita wa Jenerali Mstaafu Khalifa Haftar ambaye anahesabiwa kuu ndiye mkuu wa jeshi katika eneo la mashariki mwa Libya waliuawa jana baada ya kutokea mripuko wa bomu katika eneo la Guwarsha, magharibi mwa Benghazi.
Jumanne iliyopita pia, Baraza la Wafanyamapinduzi la Benghazi lilitangaza kuwa, wanajeshi 38 wa Khalifa Haftar wameuawa katika mapigano na askari wa baraza hilo, huko mashariki mwa Libya.
Tags