Sep 01, 2016 15:48 UTC
  • Wasiwasi wa Unicef kuhusu hali ya watoto katika eneo la Ziwa Chad

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umezitolea mwito taasisi za kimataifa kuwasaidia wahanga wa mashambulizi ya kundi la Boko Haram katika eneo la Ziwa Chad.

Unicef imetoa taarifa kuhusiana na hali waliyo nayo watoto wakimbizi katika eneo la Ziwa Chad, likiwemo suala la lishe duni kwa watoto hao na kusema kuwa inatia wasiwasi. Shirika hilo la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa limetaka kuzidishwa misaada kwa familia za wahanga wa mashambulizi ya Boko Haram.

Unicef imesema kuwa bajeti inayohitajika kwa ajili ya kuwahudumia raia hao ni dola milionii 308 na kuutaja mgogoro unaolisibu eneo la Ziwa Chad kuwa ni "Mgogoro wa Watoto." Unicef imeongeza kuwa lishe duni imezidi kuongezeka miongoni mwa watoto wakimbizi kutoka Niger, Nigeria na Chad.

Nchi za Eneo la Ziwa Chad zilizoathirika na mashambulizi ya Boko Haram

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) unatarajia kuwaslisha ripoti yake kuhusu athari za mashambulio ya Boko Haram katika nchi za Nigeria, Chad, Cameroon na Niger na kwa mara nyingine tena kuzungumzia kwa kina juu ya udharura wa kuharakishwa na kuongezwa misaada ya kimataifa kwa raia waliolazimika kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi ya Boko Haram.

Tags