Viongozi wawili wa upinzani nchini Ethiopia watiwa nguvuni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i15208-viongozi_wawili_wa_upinzani_nchini_ethiopia_watiwa_nguvuni
Duru za kuaminika zimeripoti kuwa viongozi wawili wa upinzani nchini Ethiopia wametiwa nguvuni.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Sep 12, 2016 23:45 UTC
  • Viongozi wawili wa upinzani nchini Ethiopia watiwa nguvuni

Duru za kuaminika zimeripoti kuwa viongozi wawili wa upinzani nchini Ethiopia wametiwa nguvuni.

Chama cha upinzani cha Demokrasia cha AGAW chenye makao yake katika eneo la Amhara kaskazini mwa Ethiopia kimetangaza kuwa viongozi hao wa upinzani waliotiwa nguvuni akiwemo kiongozi wa chama hicho Andualem Tilahun wamekamatwa kwa tuhuma za kuchochea umma dhidi ya serikali. Tesera Be, mmoja wa washauri wa chama cha Agaw amekanusha tuhuma hizo na kueleza kwamba kumtuhumu Tilahum kuhusika na kuwachochea wananchi dhidi ya serikali kumefanywa kwa lengo la kukifuta chama hicho katika eneo la Amhara.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Delasegn, ambaye serkali yake inatuhumiwa kukandamiza wapinzani

Chama cha Demokrasia cha Agaw ni cha kabila dogo lenye watu wapatao milioni mbili miongoni mwa jamii ya watu wa eneo la Amhara.

Andualem Tilahun na Beyilu Teshale walitiwa nguvuni tarehe 29 Agosti lakini habari za kukamatwa kwao zilitangazwa jana Jumatatu.

Hadi sasa chama cha Demokrasia cha Agaw kilikuwa hakijajihusisha na harakati za kupinga serikali za watu wa makabila ya Oromo na Amhara ambayo yanaunda karibu asilimia 60 ya watu wote wa Ethiopia.../